
Mkuu wa wilaya ya longido ndg. Daniel
G. Chongolo amezindua rasmi bodi ya afya katika Halmashauri ya wilaya
ya longido mkoani Arusha
Wakati akizindua bodi hiyo ndg. Daniel
ameeleza kuwa changamoto kubwa inayoikumba zoezi la utoaji wa huduma
ya afya ni mifumo na miundo mbinu inayotumika katika utoaji wa huduma
hiyo, huku akifafanua zaidi kuwa wilaya ya longido ina tarafa nne na
vituo vitatu vya afya viwili vya serikali na kimoja cha binafsi hivyo
kuwa na uhitaji mkubwa wa kuongeza vituo vya afya ili kukidhi mahitaji
ya watu.
Vilevile mratibu wa bodi ya afya Dr.
Justice E. Munisi ameeleza kuwa kwa upande wao wamejitahidi kutoa
huduma mbalimbali kama mafunzo ya kudhibiti ukimwi, kutoa chanjo, uzazi
wa mpango , mama na mtoto lakini wamefanikiwa kwa asilimia ndogo
kutokana na changamoto zifuatazo;1. usafiri 2.kuhama hama kwa wagonjwa
kutoka kituo kimoja kwenda kingine hivyo kuonekana kwa idadi kubwa ya
wagonjwa watoro 3. Umbali kati ya kituo cha afya na walengwa.
Hivyo basi mwenyekiti wa bodi ya afya
ndg. Isack Ole ndetero ameahidi bodi hiyo kuwa bega kwa bega
wakishirikiana na kuhakikisha kukaa vikao kwa muda na kutekeleza
mipango kwa wakati ili kutimiza malengo.