Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza
na viongozi na watumishi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya ya Ileje Mkoa wa
Songwe na Kyela Mkoani Mbeya katika ukumbi wa ofisi za Mgodi wa Kiwira
zilizopo katika Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje,
Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasili mgodini
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua hali ya mitambo tangu
kusimamishwa kwa uzalishaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mwaka
2009 katika Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje, Februari 2018.
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua hali ya magari tangu
kusimamishwa kwa uzalishaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mwaka
2009 Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje, Februari 2018.
Na Mathias Canal, Songwe
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amebainisha kuwa anajivunia
kufanya kazi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt
John Pombe Magufuli Kwani amekuwa ni kiongozi anayefanya maamuzi kwa
wakati pasina kuchelewa.
Mhe
Biteko ameyasema hayo Leo 12 Februari 2018 wakati akizungumza na
viongozi na watumishi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya ya Ileje Mkoa wa
Songwe na Kyela Mkoani Mbeya katika ukumbi wa ofisi za Mgodi wa Kiwira
zilizopo katika Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje.
Alisema
kuwa Rais Magufuli ameonyesha dhamira ya dhati ya kuepuka michakato ya
kuchelewesha maendelo kwa maamuzi ya busara na haraka anayoyafanya huku
akieleza kufurahishwa na maamuzi ya kujengwa ukuta katika machimbo ya
Tanzanite yaliyopo katika eneo la Merelani Wilaya ya Simajiro Mkoani
Arusha.
Mhe
Biteko akiwa ziarani Mkoani Songwe amemtaja Rais Magufuli kama kiongozi
mpenda haki, na msimizi madhubuti wa rasilimali za umma hivyo maamuzi
yake yamepelekea Taifa kwa sasa kufikia hatua ya kuheshimika ndani na
nje ya mipaka ya Tanzania.
Hata
hivyo alisema kuwa ili kuitafsiri vyema ndoto ya Rais Magufuli ya
kuwanufaisha wananchi kupitia sekta ya Madini amekusudia kuhakikisha
sekta hiyo inakuwa na tija kwa kukuza uchangiaji wa pato la Taifa.
Akizungumza
kwa msisitizo juu ya kusudio la serikali kuhakikisha Mgodi wa Kiwira
unaanza uzalishaji ili kuchochea ajira kwa wananchi aliutaka uongozi wa
Wilaya ya Ileje na Kyela kuketi mezani kwa ajili ya mazungumzo ya
makubaliano ya namna bora ya kumaliza sintofahamu ya namna ya ukusanyaji
mapato kutokana na mgodi huo kuwa Wilaya ya Ileje lakini baadhi ya
huduma zingine zikipatikana Wilaya ya Kyela zikiwemo makazi ya
wafanyakazi wa mgodi.
Aidha,
alisema kuwa viongozi hao pindi watakapokuwa na makubaliano mazuri
wanapaswa kutumia fedha watakazokuwa wanakusanya kwa kuzielekeza katika
miradi inayoonekana.
Sambamba
na hayo pia Mhe Biteko alielekeza Wakurugenzi kutotoza ushuru usiokuwa
na tija ambao utawafanya wawekezaji na wachimbaji kushindwa kumudu jambo
litakalopelekea kudumaa kwa faida wanayopata na hatimaye kushindwa
kuwekeza.