MASHINDANO YA UCHUMI CUP YAFUNGULIWA WILAYANI HANDENI KUHAMASISHA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA VIJANA


Katika kuhamasisha vijana kujishughulisha na shughuli za maendeleo hususani kilimo mashindano ya mpira wa mguu na mpira wa pete UCHUMI CUP yamefunguliwa rasmi kwa ngazi ya robo fainali na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mapema mwishoni mwa wiki.
Akifungua mashindano hayo kwenye viwanja vya Kigoda Stadium Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi.Upendo Magashi alisema kuwa michezo ni furaha na amani hivyo fursa hiyo itumike kukuza vipaji lakini pia kujiunga katika vikundi vya uzalishaji hususani kilimo ukizingatia Handeni shughuli kuu ni kilimo.
Aliongeza kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuhakikisha vijana wanatumia vipaji walivyonavyo katika kuhakikisha wanainua uchumi wao na kuendana na falsafa ya Mh. Rais ya HAPA KAZI TU!.
Kwa upande wake mratibu wa mashindano Bw. Baraka Nkatura alisema kuwa Mashindano yalianzishwa na Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe na kuamua kuyatumia kwenye msimu huu wa kilimo ili kuhamasisha vijana kutumia vipaji vyao kujiinua kiuchumi.
“Tunaamini mbali ya kukuza mahusiano baina yetu, tutaweza kubadilishana uzoefu utakaotusaidia kukuza vipaji vyetu na kujiinua kiuchumi” alisema Mratibu.
Upatikanaji wa timu zilizoshiriki Robo fainali ulianzia ngazi ya Tarafa tarehe 20/11/2017 ambapo, Tarafa 7 zilishiriki kutoa timu mbilimbili zilizoingia kwenye robo fainali na timu 2 alikwa moja kutoka jamii ya wamasai na ya pili kutoka Kabuku. Jumla ya timu 18 zimeingia ngazi ya mashindano ya robo fainali.
Aidha, baada ya kupatikana timu 18 kutoka kila Tarafa iliundwa mechi ya makundi kwa timu za ( Mjini Chanika kundi A, Misima B, Mkata C na Kabuku D). washindi wawili waliopatikana katika kila kundi waliingia robo fainali na kufanya timu shiriki 8.
Mpaka tarehe 4/2/2018 timu 4 zimecheza robo fainali , mchezo kati ya kurugenzi Fc na Nyikani walitoana 2-1, Ambapo Kurugenzi FC iliwafunga Nyikani FC bao 2 kwa mojo. Dakika ya 5 mchezaji John kutoka Nyikani FC alifunga goli la kuongoza na baadae mchezaji Nguruko kutoka Kurugenzi FC alisawazisha goli dakika ya 30 kabla ya mapumziko. Mchezaji Peter aliifungia Kurugenzi FC kwa shuti nje ya 18 Dakika ya 70 na kufanya bao la pili.
Mechi zinazocheza Robo fainali kwa lengo la kupata washiriki wa nusu fainali na fainali ni Kurugenzi FC vs Nyikani FC, Vibaoni United vs Kwamkono FC, Mtazamo United vs Ndolwa United na Umoja FC Vs Kwapara FC ambapo mwisho wa mashindano ya robo fainali ni 6/2/2018. Nusu fainali itachezwa tarehe 8-9/2/2018 na Finali itachezwa tarehe 11/2/2017.
Mashindano haya yamebeba kauli mbiu ya “Kipaji changu mtaji wangu” mbapo Mshindi wa kwanza atapa zawadi ya Kombe, pesa taslimu Tsh.500,000/=,medali za dhahabu, jezi seti moja na mipira mitatu. Mshindi wa pili atapata pesa taslimu Tsh.300,000/=, medali za fedha(Silva), jezi seti moja, mpira mmoja. Na mshindi wa tatu pesa taslimu Tsh.200,000/=,medali za shaba (Brons), jezi seti moja na mpira mmoja.
Washindi wa mpira wa Pete , mshindi wa kwanza atapata fedha taslimu Tsh.500,000/=, mshindi wa pili Tsh.300,000/= na mashindi wa tatu Tsh.200,000/=.

Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
 Wachezaji wa Kurugenzi FC wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza mashindano dhidi ya Nyika FC
 Timu ya mpira ya Nyika FC wakiwa tayari kuikabili timu ya Kurugenzi FC
 Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi Upendo Magashi wa kwanza kushoto, waratibu wa michezo wawili upande wa kulia wakiwa kwenye picha ya pamoja na wachezeshaji wa mpira kabla ya mechi kuanza
 Kaimu Katibu Tawala Wilaya Bi Upendo Magashi akifuatiwa na waratibu WA michezo wakisalimiana  na Timu na uongozi wao kabla ya mechi kuanza
 Mechi Kati ya Kwamkono United na Vibaoni united ikiendelea
 Timu Ya Kwamkono FC wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa michezo
 Wachezaji wa timu ya Vibaoni United wakiwa tayari kukabiliana na Vibaoni
 Mratibu WA michezo Bw Baraka Nkatula akizungumza na wachezaji wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ngazi ya Robo fainali
Kaimu katibu Tawala Wilaya Bi Upendo Magashi akifungua mashindano kwa kuzungumza na wachezaji

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post