Washiriki wa mkutano wa Wadau wa nyuki wakifuatilia mkutano kwa makini
mkutano wa masuala ya nyuki uliofanyika katika chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka
washiriki wa mkutano
Na Woinde Shizza,Kilimanjaro.
Chuo cha Usimamizi
wa Wanyamapori Mweka kilichopo Wilaya ya
Moshi Mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Wuzburg University
kilichopo nchini Ujerumani wanatarajia
kufanya utafiti wa nyuki ambao utasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo
pamoja na uhifadhi wa mazingira .
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Ladislaus Kahana alisema kuwa kutokana na umuhimu nyuki katika
uchavushaji wa mimea hivyo nyuki wanategemewa
sana katika kukuza uzalishaji wa mazao .
Ladislaus
alisema kuwa utafiti huo utafanyika katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na
baadae kufanyika katika mikoa mingine zaidi ili kuhasisha ufugaji nyuki
utakaosaidia kukuza kipato na pia kusaidia shughuli za kilimo na uhifadhi.
Mratibu wa
Utafiti wa Nyuki kutoka Idara ya Wanyamapori Mweka Dokta Oliver Nyakanga amesema kuwa utafiti huo ni wa miaka 3 kwa ufadhili wa Shirika la JRS Biodiversity Foundation lililoko nchini Marekani ,utafiti ambao utaangalia umuhimu wa
nyuki katika kilimo ,aina mbalimbali za nyuki katika aina mbalimbali za
mazingira hususan katika maeneo ya kilimo na hasa kilimo mchanganyiko.
Dokta Oliver
alisema kuwa pia utafiti huo utaangalia jinsi ambavyo matumizi ya dawa na
viuatilifu vinavyoathiri nyuki pia
ameishauri jamii ipande miti ambayo itawavutia nyuki kukaa katika maeneo hayao
kwa ajili ya uchavushaji wa maua ambayo huwa mazao.
“Tafiti
nyingi ambazo hufanyika huwa ni za wanyama wakumbwa wakubwa nyuki ni wadudu
muhimu waliosahaulika ndio maana kwa sasa tunakwenda kufanya utafiti ambao
utatupa majibu ya uhalisia ambayo yatasaidia kuwatunza nyuki kwa ajili ya
kilimo na uhifadhi” Alisema Oliver
Mtafiti
kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania Wilfred Mariale alisema kuwa
kumekua na upungufu wa nyuki kwa ujumla lakini bado hakuna taarifa za kitafiti
juu ya idadi ya nyuki
wachavushaji,kutathmini uchavushaji katika kuboresha kilimo hivyo
utafiti huo utasaidia sana .
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa masuala ya nyuki uliofanyika katika chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka.