Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza
na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi
akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa,
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Aliyenyoosha mkono) akimuonyeshaNaibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko mitambo ya uchimbaji madini alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa,
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la uchimbaji madini ya makaa ya mawe alipotembelea mgodi wa Edenville Tanzania Ltd uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa,
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Kulia) akimueleza Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko juu ya uchimbaji wa makaa ya mawe alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa,
Na Mathias Canal, Rukwa
Serikali
imesema kuwa sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2017 inaelekeza wazi kuwa Madini yote nchini ni Mali
ya watanzania hivyo wanapaswa kutambua umuhimu wa rasilimali.
Wawekezaji
na wachimbaji wote wa madini nchini wanapaswa kutambua kuwa wanalo
jukumu muhimu la kurejesha kwa jamii asilimia chache ya kile
wanachozalisha kwa kuunga mkono juhudi za serikali Back to the
Community) katika kuboresha miundombinu, sekta ya elimu, afya N.K
Naibu
Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko amesisitiza hayo Leo 23
Februari 2018 wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2,
Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika
katika eneo la mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe Mkoani
Rukwa Magharibi mwa Tanzania.
Mradi
huo unaosimamiwa na kampuni ya Edenville Tanzania Ltd kwa ubia na
kampuni ya Edenville Energy of Uk na Upendo Group (Kampuni ya kizawa)
ilianza shughuli za majaribio ya uchimbaji na uoshaji mwezi wa kumi
mwaka Jana 2017 na mkaa wa kwanza kuuzwa kwa majaribio ni mwezi Novemba
mwaka 2017.
"Nataka
niwajulishe tu watanzania wenzangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliniteua kusimamia Wizara ya
Madini nikimsaidia Waziri wetu Mhe Anjelina Kairuki ili kuboresha sekta
hii ya Madini hatimaye kuwanufaisha watanzania kuliko ilivyokuwa awali
ambapo Madini yalikuwa yanachimbwa nchini lakini faida inaenda nchi
zingine" Alisema Mhe Biteko na Kuongeza kuwa
Wawekezaji
hao wanapaswa kutoa ajira zisizo za utaalamu kwa wananchi wanaozunguka
migodi yao sambamba na watanzania wote huku akiwaagiza kuwaajiri
wataalamu wa Madini wa ndani ya nchi kwa kazi ambazo wanaweza kuzifanya
sio kuajiri wageni.
Aidha,
aliwasisitiza wananchi hao pindi wanapopata ajira zao katika migodi
mbalimbali wanapaswa kuwa waaminifu ili kuwavutia wawekezaji hao jambo
litakalopelekea wawekezaji kuwa na imani na watanzania na hatimaye
kuongeza chachu ya ajira nyingi zaidi.
Sambamba
na hayo amekemea baadhi ya wafanyakazi katika migodi mbalimbali ambao
wameaminiwa na kupatiwa ajira lakini wanageuza muda wa kazi kuwa muda wa
starehe kwa kunywa pombe na utoro kazini.
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko yupo katika ziara ya kikazi ya
siku mbili Mkoani Rukwa kutembelea na kukagua uchimbaji wa Madini.