washiriki
wakijiandaa tayari kwajili ya kuanza mashindano wakiwa pamoja na Naibu
waziri wa maliasili na utalii Mh, Lazaro Nyalandu pamoja na waandaaji
Mh, Lazaro Nyalandu akimtoka Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mheshimiwa Anthony Mtaka katika mbio hizo
mwimbaji wa bongoflava Barnaba akiwa na Irene Kiwia manager director
kutoka Frontline Porter Novelli ambaye pia alikuwa mshiriki wa miss
Tanzania wakishiri mbio hizo ambapo walimaliza mbaka mwisho.
Mshindi
wa kwanza kwa upande wa wanawake bi Jacquline Salum toka Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akiwatoka washiriki wenzie
Bwana Dickson akihojiwa na wandishi wa habari baada ya kushinda mbio hizo
Naibu waziri wa Mali asili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabizi zawadi kwa mshindi wa kwanza bwana Dicksoni Marwa.
Dickson
Marwa alijichukulia kitita cha shillingi millioni moja za
kitazanzania baada ya kuibuka mshindi wa Tigo Ngorongoro nusu
Marathon ambapo mshindi wapili bwana Stephano Huche ambae nae ni
aliweza kuondaka na kitita cha shillingi laki tano.
Mashindano
haya ambayo lengo lake ni kuhamasisha mapingano dhidi ya ugonjwa wa
malaria yameandaliwa na taasisi tanzu ya kujitolea ya kampuni ya Utalii
ya ZARA Tanzania Adventures ambayo husaidia shughuli mbalimbali za
kijamii kwa kujitolea na kudhaminiwa na kampuni ya Tigo.
akizungumza
na waandishi wa habari Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Lazaro
Nyalandu alisema kila hatua moja ambayo atakuwa anakimbia mkimbiaji
itakuwa inahamasisha umoja katika kupambana na malaria hatua hiyo pia ni
ishara inayoonyesha nia njema ya waandaaji wa mbio hizo kutokana na
lengo la kupambana na ugonjwa huo hatari unaoua wananchi wengi
"Kwa
takwimu tulizonazo hadi sasa ni kwamba malaria inaua watu zaidi 888,000
barani Afrika na robo tatu wa watu hao ni watoto wenye umri chini ya
miaka mitano na kwa hali hiyo, mbio hizi zinachagiza uhamasishaji wa
kupambana na ugonjwa huo" alisema
Mbio hizo ambazo
zinafanyika kila mwaka zimeshirikisha vilabu 26 kutoka Tanzania nzima
zilizo na wanariadha 236, zilianzia katika geti la kuingilia kwenye
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kumalizikia katika uwanja wa Karatu
mjini.
Kwa upande wa wanawake, mwanariadha Jacquline
Salum toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliibuka
mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano, akifuatiwa na
Zakia Mrisho aliyejinyakulia shilingi laki tatu.
Akizugumza
Mkurugenzi wa Zara Tours Leila Ansell ambao ni waaandaaji wa mashindano
hayo alisema mashindano ya Mwaka huu wamepata washiriki wengi zaidi ili
kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kupambana na ugonjwa na Maralia
pia ni kuunganisha pamoja watalii na wananchi wa Tanzania pamoja na
kukusanya fedha zitakazotumika katika mapambano ya ugonjwa hatari wa
Malaria.
Aidha mashidano hayo yalianza mapema saa
12:00 asubuhi leo kwa mbio za watoto kuazia eneo la Mnadani, Karatu,
mbio za wakubwa za km 21 zilianzia geti kuu la Ngorongoro na kumalizikia
viwanja vya mazingira bora Karatu
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia