SAKATA la mkazi wa Kijiji cha Madunga,Kata ya Madunga Wilaya ya
Babati Mkoani Manyara,kuwaingilia mbuzi wa eneo hilo,limechukua sura mpya baada
ya mmoja kati ya mbuzi aliowaingilia kuharibika mimba.
Akizungumza juzi,mmiliki wa mbuzi huyo Clementina Masay alisema
mtuhumiwa huyo ambaye amekuwa akiwabaka mbuzi na kuwaingilia kwa nguvu
amemsababishia hasara baada ya mimba ya mbuzi wake jike kuharibika.
Masay alisema kuwa Serikali inatakiwa imchukulie hatua kali
mtuhumiwa huyo kwani baada ya kufikishwa Mahakamani na kufunguliwa kesi alipata
dhamana lakini hadi hivi sasa ametorokea sehemu isiyofahamika.
Alisema mtuhumiwa huyo,Daniel Marcel (22) alifunguliwa kesi namba
29/2013 kwa kosa la kuiingilia mifugo,kinyume na kifungu cha 325 kanuni ya
adhabu sura ya 16 na alipopata dhamana akatoroka.
Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Julius Dagharo wa Mahakama ya Mwanzo
Bashnet,ambaye ndiye aliyemsomea shtaka na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho Omari
Mwanditi alikiri mshtakiwa huyo kutoroka baada ya kupatiwa dhamana.
Jamii ya wafugaji wa kiiraq wa eneo hilo wamesikitishwa na kitendo
cha mifugo yao kuingiliwa mara kwa mara kwa kunajisiwa na walidai kuwa
watamsaka mtuhumiwa huyo hadi wamkamate kwani kitendo hicho kimewasikitisha.
Hata hivyo,walidai kuwa matukio ya mtuhumiwa huyo kuwaingilia
mifugo yamekuwa yakitokea mara kwa mara na pindi anapoulizwa anadai kuwa
anaiingilia mifugo kwa kuogopa kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia