Sensei Rumadha Fundi (Romi) mtaalam wa ngazi za juu wa karate na Yoga ,
Tunapozungumzia
watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na
kuviendeleza vipaji hivyo hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la
Sensei Rumadha Fundi aka Romi
hatuwezi
kulikwepa,mtanzania mwenye makazi yake nchini marekani,kabla ya
kujikita kule marekani alikuwa moja ya wanafunzi wa karate pale
Zanakaki,Dar chini ya mwalimu wake
Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP), baada ya hapo akaenda kwa mafunzo zaidi nchini Japan,Sweden na Denmark,
akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa
mtaalamu wa Yoga,Vipaji hivi vya Karate na Yoga ,Sensei Rumadha Fundi
anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji .Sensei Rumadha Fundi
ni mwalimu wa karate na yoga
mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana,tena mwenye nidhamu.
Sensei
Rumadha Fundi (Romi)( 3rd Dan black belt), akiwajibika katika semina
ya karate Dojo ya Sugarland, Texas USA katika seminar ya walimu wa
karate (ma-sensei) wiki iliyopita chini ya uongozi wake Sensei Ramon
Veras (7th Dan), wa Traditional Okinawan Goju Ryu Karate-Do.Sensei Rumadha ni mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii ughaibuni, ni matumaini yetu wahusika katika sekta ya michezo hasa upande wa mapambano kama ngumi, kick boxing, judo nk wataangalia uwezekano wa kupata mchango wao ambao unaweza kusaidia katika kuboresha wanamichezo wetu kufikia kiwango cha kimataifa na kuliletea sifa taifa letu.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia