Umati mkubwa wa wanafunzi wa chuo
cha uhasibu njiro jijini Arusha wakiwa wanamsikiliza kwa makini Mbunge
wa Arusha mjini Godbless Lema mara baada ya kuandamana kutokana na
mwenzao kuuwawa kikatili na watu wasiofahamika usiku wa juzi
Mkuu wa mkoa Magessa Mulongo
pamoja na timu yake wakiingia katika eneo la shule ambapo aliambulia
zomea zomea ,kurushiwa mawe,lugha za kejeli kutoka kwa wanafunzi hao kwa
kile wanachodai kuwa serikali imekuwa siyo sikivu kutatua matatizo yao
ya mara kwa mara ikiwepo kuibiwa vitu mbalimbali
Askari wakiwa tayari kukabiliana
na wanafunzi hao waliosababisha vurugu huku Mbunge Lema akisakwa na
jeshi la polisi kwa tuhuma za kuchochea vurugu hizo
MWANAFUNZI
wa mwaka wa pili katika chuo cha uhasibu kilichopo Njiro jijini
Arusha,Henry Koga anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (25 hadi 30)
ameuawa kinyama kwa kuchinjwa na kisu shingoni na kundi la watu
wasiofahamika wakati wakitoka kwenye kumbi za starehe na wenzake.
Kufuatia
tukio hilo ,kundi la wanafunzi walileta vurugu kubwa na kukataa kutii
amri ya mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ya kuwataka warudi
darasani wakati hatua zaidi za kisheria zikichukuliwa huku
wakimzomea,hali iliyosababisha polisi kuingiliaka kali na kuwafyatulia
mabomu zaidi ya 50 na baadhi yao kujeruhiwa.
Tukio
la kuuawa kwa mwanafunzi huyo limetokea majira ya saa 4 usiku wa
kuamkia leo ambapo marehemu huyo akiwa na wenzake walivamiwa na kundi la
wahuni wapatao wanne katika eneo la CDA ,umbali mchache kutoka eneo la
chuo hicho na kumchoma kisu shingoni .
Hata
hivyo jitihada za wenzake kutaka kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza
hospitalini, zilishindikana kwani alifariki dunia muda mfupi baada ya
tukio hilo kutokana na kuvuja damu nyingi.
Aidha
wanafunzi hao walijikusanya asubuhi yake na kuanza kuandamana
kushinikiza uongozi wa chuo hicho kutoa tamko juu ya vitendo vya
uhalifu vinavyojirudia mara kwa mara katika chuo hicho bila kuchukuliwa
hatua zozote na kufanya maisha ya wanachuo hao kuwa hatarini.
Wanafunzi
hao walisikika wakilalamikia hali ya ukimya wa viongozi kushindwa
kudhibiti matukio ya uhalifu kwani mwishoni mwa mwaka jana mwanafunzi
mwingine aliuawa na vibaka kwa kuchomwa na kisu pia wanafunzi hao
waliwahi kuvamiwa chuoni wakiwa wamelala na kuporwa vitu mbalimbali
ikiwemo laptop simu na fedha.
Wakati
vurugu za wanafunzi zikiendelea alifika mkuu wa mkoa wa Arusha ,Magesa
Mulongo na kuwasihi waache vurugu na wakubali kumsikiliza hata hivyo
wanafunzi hao zaidi ya 500 walianza kumzomea huku baadhi yao wakionekana
kurushia mawe
Mkuu wa
mkoa alilazimika kuondoka eneo hilo ,hatua iliyowalazimu askari wa
kutuliza ghasia kufyatua mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya na
kujikuta baadhi yao wakijeruhiwa vibaya .
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ,Ibrahimu Kilongo alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanafunzi zaidi ya 7 wanashikiliwa
katika vurugu hizo huku uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea .