Machimbo ya moram yaliyoko moshono mkoani Arusha yaliyosimishwa na serikali kwa mda |
Serikali imesimisha kwa muda machimbo ya morom yaliyoko
katika kata ya moshono jijini Arusha baada ya kusababisha vifo vya watu 13 na
majeruhi 2 lengo ikiwa ni kutathmini mazingira ya machimbo hayo kwa kuwa ni
muhim kwa shughuli za ujenzi wa mkoa huu na jirani.
Hayo yameelezwa na Waziri mkuu Mizengo Pinda wakati
akihudhuria ibada maaalum ya kuaga miili ya marehem walikufa katika machimbo
hayo sambam,ban a kuyatembelea mapema
leo mkoani Arusha
Waziri Pinda pia alipata fursa ya kutembelea majeruhi hao na
kutembelea eneo la tukio sambamba na kuzungumza na wakazi wa eneo hilo na
kuwapa pole wafiwa na kusisitiza kuwa hawajafunga machimbo hayo bali
yamesitishwa kwa muda kwa ili kuboresha mazingira ya machimbo nah ii ni katika
kutambua umuhimu wa nishati hiyo ya madini ya ujenzi pamoja na kipato kwa
wakazi wa eneo hilo.
Kwa upande wake naibu
waziri wa nishati na madini Stevin Masele aliwapa pole wahusika na kusema kuwa
vifo hivyo vimesababishwa na ukosefu wa elim ya uchimbaji wa madini hayo hivyo
kuonya viongozi wa serikal I kutootoza ma;pato katika sehem ambazo hazina
laseni wala kuruhusiwa na serikali kwani yana chochea uchimbaji holela na
kusababisha maafa kwa kutozingazita sheria.
Aidha alisema kuwa kwa niaba ya wizara waataanda semina ya
mafunzo kwa wachimbaji wadogo wadogo ili kuweza kuwajengea uwezo wa kutambua
sheria na tarartibu za uchimbaji ambazo serikali itatoa baadhi ya vifaa vitakavyowasaidia
katika uchimbaji huo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia