Katibu
wa Kikundi cha Ujasiriamali cha mkorofi si mwenzetu akipokea mchango wa
shilingi 300,000 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa
jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM ndugu Sadifah
Juma.
Akina
Mama waliojitokeza katika Mkutano wa Jimbo la Donge, ambapo Mwenyekiti
wa UVCCM Taifa na Mbunge wa Jimbo hilo Sadifah Juma alikabidhi michango
ya fedha taslimu na vifaa vyenye jumla ya kiasi cha shilingi milioni
nne.
Mwenyekiti wa Jimbo la Donge, Ally Maabad akiwa katika mkutano huo ambao Mbunge wa jimbo la Donge Mhe. Sadifah Juma alichangia vikundi mbalimbali vya ujasirimali. |
Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Taifa, Ndugu Martine Shigela akiwa
anazungumza na kusisitiza jambo katika mkutano huo ambapo alisema kuwa
wananchi wa Jimbo la Donge wanayo bahati ya kuwa na mbunge anayewajali
na kusaidiana nao katika kulijenga na kuliletea maendeleo jimbo la
Donge.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na mbunge wa jimbo la Donge Mheshimiwa Sadifah
Juma, amefanya mkutano wa hadhara jimboni humo ambapo amechangia takribani
shilingi milioni 4, ikiwemo pesa taslimu shilingi milioni tatu na laki mbili
(3,200,000) pamoja na vifaa vya ushoni vyenye thamani ya shilingi milioni 1 kwa
vikundi mbalimbali vya ujasiriamali vya jimboni Donge.
Sadifah amechangia kiasi hicho kwa vikundi
12 vya ujasiriamali ambapo vikundi 4 vya ufugaji wa kuku wa kisasa vilipatiwa
kiasi cha shilingi laki 300,000 kila kimoja,vikundi hivyo ni Inshaallah
Hatuchoki, Letu moja , Sisi kwa sisi na kikundi cha Mkorofi si mwenzetu. Mbali
na vikundi hivyo pia vikundi vya utengenezaji matofali, vikundi vya ushonaji na
vikundi vya kukopeshana vilinufaika na michango ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe.
Sadifah.
Katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa
na viongozi waandamizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) kutoka Makao Makuu ya Jumuiya hiyo wa afisi kuu ya Zanzibar na Dar es
salaam wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja huo Ndugu Shigela Martine, Makatibu
wa Idara za Jumuiya hiyo na maafisa wa Makao Makuu, Mheshimiwa Sadifah
ameichangia timu ya mpira wa miguu ya Kata ya Vijibweni-mahonda vifaa vya
michezo.
Mbali na michango hiyo ya fedha taslimu na
nyenzo za kimaendeleo, Mhe. Sadifah amesisitiza vijana wa jimbo hilo kujituma
kwa hali na mali katika kujiletea maendeleo binafsi na pia kushiriki katika
shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo jimboni humo, akasisitiza
kuthamini na kuvitunza vifaa vlivyotolewa katika vikundi hivyo na kuvitumia
ipasavyo ili viweze kuwa msaada endelevu kwa vikundi hivyo.
Nae, Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu
Martine Shigela aliwasisitiza Vijana kuwa msitari wa mbele katika kushiriki
shughuli mbalimbali za mendeleo na kuwa mfano bora wa kufanikisha na kutekeleza
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, lakini pia akawaahidi Vijana wa jimbo hilo kuwa
Jumuiya ya Vijana itawasaidia katika kuwapa mafunzo ya ujasiriamali ambayo
Jumuiya hiyo inayatoa kwa vijana mbalimbali hapa nchini ili kuwawezesha
kushiriki shughuli za kimaendeleo na ujasiriamali kwa uhakika na ufanisi zaidi.
Mheshimiwa Sadifah yupo jimboni humo katika
ziara mbalimbali za kumuenzi muasisi wa Mapinduzi-Marehemu Abeid Aman Karume,
aliyefariki tarehe 06th April 1972, ambapo kilele cha maazimisho ya
kumbukumbu hizo yatafanyika katika afisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi iliyopo
kisiwandui mjini unguja
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia