CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo(Chadema) mkoani Arusha kimelalamikia kitendo cha
uongozi wa halmashauri ya jiji la Arusha kukosa mkurugenzi wa kudumu katika
ofisi hiyo kwa takribani miaka mitatu hadi sasa.
Hadi sasa
halmashauri ya jiji la Arusha haina mkurugenzi kamili baada ya aliyekuwa kaimu
wake,Omary Mkombole kuhamishiwa wilayani Babati kuwa mkurugenzi kamili na kwa
sasa inakaimiwa na mhandisi mkuu,Afwilile Lamsy.
Akitoa tamko
hilo juzi mwenyekiti wa madiwani wa Chadema jijini hapa,Isaya Doita alisema
kuwa inashangaza ofisi ya jiji hilo kukaimiwa kwa miaka mitatu hadi sasa bila
kuwa na mkurugenzi kamili.
Alisema kuwa
cha ajabu ofisi ya mkurugenzi wa jiji la Arusha imekuwa ikitumiaka kuandaa
wakurugenzi mbalimbali wanaopitia Arusha na kwenda kuwa wakurugenzi katika
maeneo mengine nchini.
Doita,ambaye
pia ni diwani wa kata ya Ngarenaro jijini hapa alitolea mfano wa makaimu
wakurugenzi ambao wamepitia jijini hapa na kwenda kuwa wakurugenzi kamili ni
pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya Mpanda,Estomi Chang”a sanjari na
mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati,Mkombole.
“Tunapinga
kitendo cha halmashauri yetu kutumika kama kituo cha kuandaa wakurugenzi
wanaopelekwa katika maeneo mengine nchini ihali sisi tunabaki na makaimu tu”alisema
Doita
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia