Mkurugenzi wa shirika la PINGO’S
Edward Porokwa akisoma tamko kwa wanahabari jijini Arusha tamko
lililoshirikisha mashirika 13 yasiyokuwa ya kiserikali juu ya mgogoro
mkubwa wa ardhi unaondelea Loliondo
Jovitha Mlay kutoka (TGNP)aliyevalia nguo nyekundu alisoma tamko kwa wanahabari
Onesmo Olengurumwa Mtetezi wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania(THRD)akisoma tamko
MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali
13 hapa Nchini wanaotetea haki za binadamu kwa pamoja wametoa tamoko lao
kuhusu mgogoro mkubwa wa ardhi unaoendelea Loliondo dhidi ya mwekezaji
OBC huku wakimtaka Waziri wa mali asili na utalii kuacha kupotosha umma
wa watanzania juu ya mgogoro huo
Hatua hiyo imekuja baada ya hivi
karibuni waziri wa mali asili na utalii Mh.Balozi khamisi Khagasheki
kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari kuwa serikali imeamua
kupunguza ukubwa eneo hilo ili kutatua migogoro iliyopo katika eneo
hilo kunusuru ikolojia ya hifadhi ya Serengeti,Ngorongoro na Pori
tengefu la Loliondo
Watetezi hao kwa pamoja walitoa
tamko hilo jijini Arusha tarehe 4/4/2013 ambapo Mkurugenzi wa shirika la
PINGO’S Edward Porokwa akisoma tamko kwa wanahabari alisema kuwa
upotoshaji huu umekuwa na lengo la kuwaahadaa umma wa Watanzania na
ulimwengu kwamba eneo lote la loliondo ni eneo la hifadhi pekee na siyo
ardhi ya vijiji hivyo wananchi kuonekana ni wavamizi jambo ambalo si
lakweli
Alisema kuwa nia ya serikali
kuwaondoa wananchi katika maeneo yao ya vijiji vyao kumekuwepo na hatari
kubwa ya wizara kutumia mbinu za kumega na kupokonya kilomita za mraba
1500 ya ardhi ya vijiji na kuikabidhi kampuni ya OBC kwa kisingizio cha
kuwagawia sehemu ya pori tengefu la loliondo huku akidai kuwa siyo
sahihi kwa kuwa ni ya vijiji husika
“Wanahabari Ardhi ambayo
Serikali inasema imewaachia wananchi ni ardhi ya vijiji vilivyopo katika
mipaka na katika hili, Serikali imepokonya ardhi yenye ukubwa wa
kilometa za mraba 1,500 na kumpatia mwekezaji wa OBC”alisema
Kwa upande wake , Jovitha Mlay
kutoka (TGNP)alisema kuwa uamuzi wa serikali wa kugawa eneo la vijiji na
kulifanya kuwa pori tengefu unachochea mgogoro uliopo kwa sasa huku
akisisitiza kwamba siyo kweli kuwa serikali ina lengo la kuinusuru
ikolojia ya hifadhi ila nia yake ni nikumpatia mwekezaji OBC.
“Hii haina ukweli wowote kwani
serikali wasingeruhusu uwindaji ufanyike kama wangekuwa na uchungu wa
kuwalinda wanyama pamoja na ikolojia hiyo”alisema Mlay
Naye Mtetezi wa watetezi wa haki
za binadamu Tanzania Onesmo Olengurumwa alisema kuwa serikali iache
mara moja mpango wake wa kugawa ardhi ya wananchi kwa manufaa ya
mwekezaji kwa kisingizio cha manufaa ya umma
“Naomba serikali iache mara moja
kuptosha umma kuwa ardhi hiyo siyo ya vijiji na izingatie sheria kwa
kuvipa vijiji haki ya kuamua mambo yao kwa kuzingatia sheria za serikali
ya mitaa”
Mashirika hayo yaliyotoa tamko
ni PINGO’S Forum,TALA,Haki Ardhi,LHRC,Tanzania human Rights
Defendes,TGNP,TNRF,Cords,CRT,PWC,NGONET,TPCF,OSEREMI
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia