Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna Jenerali John Minja, akikata utepe kuzindua rasmi jukumu la
kuwasafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi
Gerezani kwa Mkoa wa Arusha. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu
Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere akipongeza uzinduzi huo. Uzinduzi huo
ulifanyika katika Gereza Kuu Arusha.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akisalimiana na Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere baada ya kutoa hotuba ya
uzinduzi wa mabasi manne na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya
kuwasafirishia mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi
gerezani kwa mkoa wa Arusha. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu
Arusha.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mabasi
manne na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia mahabusu
toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa Mkoa wa Arusha.
Katika hotuba yake mkuu wa jeshi hilo aliwataka maofisa magereza wa mkoa
huo wawe makini kuyatunza magari hayo. Uzinduzi huo ulifanyika katika
Gereza Kuu Arusha.
Sehemu
ya magari matano ya kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Mkuu wa
Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, katika hafla
iliyofanyika Gereza Kuu la Arusha.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia