-Tume ya kitaifa inatarajiwa kuanza kuchunguza kashfa za udhahlilishaji wa watoto kingono mjini Melbourne, Australia.
Zaidi ya watu 5,000 wanatarajiwa kutoa ushahidi wa dhulma hizo na kuelezea athari walizopata.
Waziri mkuu Julia Gillard, ameonya kuwa tume hiyo itaweza kuibuka na ukweli ambao kwa baadhi ya watu huenda ikawa kero kubwa.
Alisema kuwa ufunguzi rasmi wa tume hiyo ni hatua muhimu ya kimaadili kwa Australia.
Tume hiyo itachunguza makundi ya kidini , asasi
za kijamii na wahudumu wa afya wa serikali,pamoja na mashirika mengine
ya serikali.
Lakini maafisa wa tume hiyo wameonya kuwa huenda wasikamilishe kazi yao ifikapo mwaka 2015 kama wanavyotakiwa.
Walisema kuwa ni kwa sababu ya wingi wa kesi
walizopokea, ikilinganishwa na idadi ya watu wanaotarajiwa kutoa
ushahidi wao na idadi ya tasisi zilizoshtumiwa.
Uchunguzi utaangalia majibu ya taasisi zilizoshutumiwa kuhusika na kuwaharibu watoto au kuwadhalilisha kingono.
Kuundwa kwa tume hiyo, kulitangazwa na waziri
mkuu Bi Gillard mwezi Novemba kufuatia shinikizo kutoka kwa wabunge
baada ya madai ya polisi kuwa kanisa katoliki lilifutilia mbali ushahidi
wa makasisi waliowaharibu watoto.
Bi Gillard alisema kuwa anataka tume hiyo kutoa
uponyo kwa waathiriwa wa vitendo hivyo, kwa sababu kwa muda mrefu wengi
wa waathiriwa hawajapata msaada
Visa vya kuwaharibu watoto, vinavyofanywa na makasisi vimekuwa swala tete nchini Australia katika miaka ya hivi karibuni.
Mwezi Septemba, kanisa katoliki katika jimbo la
Victoria walithibitisha kuwa zaidi ya watoto miasita waliharibiwa na
makasisi tangu mapema miaka ya thelathini.
Wakati wa ziara yake nchini Australia mwaka
2008, Papa mstaafu Benedict, alikutana na baadhi ya waathiriwa na koumba
msahama hadharani.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia