POLISI wa kike wa Kituo cha Magomeni, jijini Dar es
Salaam aliyejulikana kwa jina moja la Anisa, ametimuliwa kazi kwa madai ya
kupiga picha ya utupu iliyosambaa mitandaoni.
Chanzo makini ndani ya jeshi hilo kilisema Anisa
alifukuzwa kazi wiki iliyopita baada ya kuhojiwa na mabosi wake wa makao makuu
ya jeshi hilo na kukiri kuwa picha hiyo ni yake.
“Anisa aliitwa makao makuu,
mabosi wakamuonesha picha yake akiwa mtupu kitandani, akakiri ni yeye.
Alijitetea eti alifanya hivyo kwa sababu siku ya tukio alikuwa amelewa
sana,” kilisema chanzo.
Chanzo kiliendelea kudai kwamba baada ya afande huyo
mwenyeji wa Tanga kukiri, viongozi wa jeshi hilo walimwambia amekiuka kanuni na
kulidhalilisha jeshi hilo hivyo hataendelea kuwa mtumishi.
Picha ya afande huyo imeenea mitandaoni na kwenye
baadhi ya simu za mikononi za watu kitendo kulicholifanya jeshi hilo kufanya
uchunguzi na kubaini kuwa ni yake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Kamishina, Suleiman Kova alipoulizwa juzi alikiri kufukuzwa kwa askari huyo na
kumtaka mwandishi wetu kufuatilia zaidi kwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni, ACP Camilius Wambura ambaye naye alipoulizwa kuhusu tukio hilo
alikiri.
‘‘Tunahitaji askari wenye
maadili mema ndani ya jeshi letu, yule atakayefanya mambo bila kufuata kanuni na
sheria hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Askari muda wote anatakiwa awe mfano
bora kwa jamii,’’ alisema Afande Wambura.
Taarifa zaidi zinadai kwamba kwa sasa Anisa anaishi
uraiani kama raia wa kawaida