WATU wawili ambao ni wafuasi
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , waliofariki jana baada ya
kulipukiwa na bomu katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Udiwani kata
ya Kaloleni,jijini Arusha, mmoja ametambuliwa na mwingine bado
hajafahamika.
Mganga, mfawidhi wa hospital
ya mkoa wa Arusha, Dakta Josiah Mlay, amemtaja marehemu huyo kuwa ni Judith
Mushi, (46) mkazi wa Sokon one jijini Arusha, na mwingine ni kijana wa kiume
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 15-16 ambae hajafahamika ambae
alifia hospital ya AICC.
Dakta Mlay, amesema katika
tukio hilo
hospital hiyo imepokea majeruhi 10 kati ya 15 na wote ni wanaume
isipokuwa majweruhi mmoja wa kike aitwae Sharifa Jumainne ,ambae hali
yake ni mbaya.
Amesema kuwa katika uchunguzi
wa awali imegundulika kuna kuipande cha chuma kwenye mapafu ambacho kinatokana
na mlipuko wa bomu
Aidha amesema kuwa majeruhi
mwingine aliyepata majeraha ya kichwa amehamishiwa kwenye hospital ya
Seliani ya Arusha kwa uchunguzi zaidi akisubiriwa kupelekwa hospital ya
rufani ya KCMC ya mjini Moshi.
Dakta Mlay, amesema hali za
majeruhi wengine waliolazwa hospital ya mkoa wa Arusha ya mount Meru,
zinaendelea vizuri.
Wakati
huo huo tume ya taifa ya uchaguzi jimbo la Arusha, imeahirisha uchaguzi huo
hadi June 30 mwaka huu kutokana na tukio hilo
la mripuko wa bomu lililojeruhi watu .
Katika
hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, amewatembelea majeruhi
wa mlipuko huo waliolazwa katika hospital mbalimbali za mkoani Arusha zikiwemo
mount Meru, Seliani, na AICC .
Katika hatua ingine viongozi
mbalimbali w a chadema wametembelea katika eneo la tukio akiwemo mwenyekiti wa
chama cha demokrasia na maendeleo chadema Freeman Mbowe na wabunge wa jimbo la
Arumeru pamoja na Arusha mjini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia