Kamishina wa polisi Paulo Chagonja akiongea na waandishi wa habari
Jeshi la
polisi linawasaka Mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe pamoja
na Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa kosa la kuendesha mkutano wa hadhara bila
kibali .
Aidha pia
jeshi hilo linawashikilia watu 67
wakiwemo wabunge wanne wa kambi ya upinzani
kwa kosa la kufanya mkusanyiko usikuwa na kibali katika kiwanja cha Soweto
jijini hapa.
Akiongea na
waandishi wa habari kamishina wa polisi Paul Chagonja Alisema kuwa wanawasaka
wabunge hao baada ya kukimbi kusiko julikana mapema jana mara baada ya kufanya
mkutano pasipo kuwa na kibali mmiliki wa kiwanja(AICC) pamoja na jeshi la
polisi .
Aliwataja wabunge ambao wamekamatwa na jeshi hilo kuwa ni pamoja na mbunge wa singida Tundu
Lissu ,Mbunge viti maalumu Joyce Nkya,mbunge wa Mbulu Mustafa Akunay pamoja na
Saidi Arifu ambapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema kesho mara baada
ya kupata mthamana wakiwa katika kituo kikuu cha polisi mkoa
Sanjari na
hilo pia kamishina huyo alisema kuwa jeshi hilo linawataka viongozi hao wawili wa
kambi ya upinzani kuja kutoa ushaaidi wa mlipuko wa bomu uliotokea Jun 15 katika kiwanja cha Soweto wakati
mkutano wa chadema wa kufunga kampeni ulipokuwa unafanyika kwani viongozi hao
walidai kuwa wanao ushaidi wa kutosha wa picha na video zinazoonyesha muhusika
wa kitendo hicho cha ulipuaji
“kama kweli
mbowe na lema wanamapenzi mema na wakazi wa Arusha na uchungu wa damu ya
wananchi iliyomwagika wajitokeze kulisaidia jeshi la polisi kutoa ushaidi huo
,ili muhusika aweze kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwani polisi sio wauaji
bali wasimamia ulinzi na haki ya wananchi wake na kama basi wataona hawataki
kutoa ushaidi kwetu na wanatuisi vibaya kama wanavyo sema basi wapeleke ushaidi
huo kwa Rais wa nchi maana yeye ndie
Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya
ulinzi na usalama hapa nchi”alisema Chagonja
Aliongeza
kuwa kama wataona pia huko apafai kupeleka
basi watafute shehe au padre wapeleke ushaidi huo na hatu kali za
kisheria zitachukuliwa kwa mtu huyo ambaye ameusika ,aidha alibainisha kuwa
endepo hawata fanya hivyo sheria itafata mkondo wake kama inavyosema kuwa iwapo
mtu anaushaidi wa kosa la jinai na anakaa nao pasipo kuutoa kwa vyombo vya dola basi mtu Yule nae
atachukuliwa sheria ya yeye pia kufunguliwa kosa la jinai.
Pia
aliwataka wakazi wa mkoa wa Arusha kuendela na shughuli zao huku wakijipusha na
makundi ya kisiasa pamoja na mikusanyiko isiyokuwa na kibali kwani kufanya ivyo ni kuendeleza machafuko
huku wahusika wakiwa wanatafuta mkono wao kwenda kinywani .
Aidha
aliwataka waandishi wa habari kuwa wazalendo kwa nchi yao na kutumia
kalamu pamoja na kamera zao kulinda na
kutunza amani ya nchi ikiwemo
kuheshimimu sheria kwa kuandika habari za kweli zenye kulinda amani
kuliko kuleta machafuko.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia