Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib
Billal akihutubia wananchi katika viwanja vya sabasaba Mji mdogo wa
Namanyere Mkoani Rukwa katika kuhitimisha siku ya mazingira duniani
ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Rukwa tarehe 05.06.2013. Katika hotuba
yake hiyo alisisitizia juu ya uhifadhi wa mazingira kwa kutunza vyanzo
vya maji, milima na misitu ya asili, kuhifadhi ardhi na kupanda miti
katika maeneo yaliyoathirika na usafi wa mazingira kwa ujumla.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikagua kitalu cha miche ya miti
mbalimbali ya mjasriamali ndugu Kidevu (kushoto) katika maonyesho kwenye
kilele cha siku ya mazingira kitaifa Mkoani Rukwa katika Mji mdogo wa
Namanyere wilayani Nkasi tarehe 05.06.2013, Kulia ni Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akisoma moja ya vitabu vya uhifadhi
wa mazingira wakati akikagua banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira kwenye kilele cha siku ya mazingira kitaifa Mkoani Rukwa
katika Mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi tarehe 05.06.2013, Kulia
kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa
wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib
Billal akimkabidhi kikombe na cheti Ndugu Leonard Kapini Makamu
mwenyekiti Halmashauri ya Mji Mpanda kwa Halmashauri hiyo kuwa mshindi
wa kwanza kitaifa katika usafi wa Miji nchini. Zawadi nyengine
waliyopewa ni Pikipiki moja. Jiji la Nyamagana limekuwa la kwanza
kitaifa na Manispaa ya Moshi ikiwa Manispaa ya kwanza kitaifa katika
usafi wa Mazingira mwaka huu 2013
Baadhi
ya viongozi na wafanyakazi wa Halmashauri ya Mji Mpanda wakifurahia kwa
pamoja ushindi kwa halmashauri yao kuwa ya kwanza kitaifa katika usafi
wa Miji nchini mwaka 2013. Halmashauri hiyo imezawaidiwa cheti, kikombe
na pikipiki moja.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikagua mtambo asilia wa kuzalisha
umeme kwa kutumia upepo uliobuniwa na mjasiriamali kutoka Mkoani Rukwa
wa kampuni ya Ulaya Hydro and Windmill Technology (Kulia), Katikati ni
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Kulia ni Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa
wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima mara baada ya kuwasili kwa helkopta
katika viwanja vya Sabasaba katika Mji mdogo wa Namanyere Wilayani Nkasi
kwa ajili kushiriki katika kilele cha siku ya mazingira duniani ambayo
kitaifa imefanyika Mkoani Rukwa.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akipanda mti wa kumbukumbu katika
kampeni ya uhifadhi wa mazingira mbele ya Ofisi ya Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi tarehe 05.06.2013 ikiwa ni kuadhimisha
siku ya mazingira duniani ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Rukwa.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akizindua kwa kuwasha mashine mpya
ya maji katika bwawa la maji Mphiri ambalo ni chanzo kikuu cha Maji
katika Mji mdogo wa Namanyere Wilayani Nkasi tarehe 05.06.2013. Serikali
imetenga jumla ya Tshs bilioni nne (4) kuendeleza chanzo hicho muhimu
ambacho asili yake ni chemchem.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa
akihutubia wananchi ambapo alikemea uharibifu wa vyanzo vya maji na
kuwaasa wanasiasa kutofanya siasa zitakazopelekea kuhatarisha uhai wa
vyanzo vya maji kwani umuhimu wa maji hauna mbadala.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kuwatambulisha
baadhi ya viongozi wakuu waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mazingira
duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Rukwa.
Naibu
Waziri wa Afya Dkt. Seif Suleiman Rashid akiwataja washindi mbalimbali
wa usafi wa mazingira kitaifa katika ngazi ya majiji, manispaa, miji na
wilaya ambao walipewa zawadi mbali mbali. Walioongoza ni Halmashauri ya
Jiji la Nyamagana (Majiji), Halmashauri ya Manispaa ya Moshi (Manispaa),
Halmashauri ya Mji Mpanda (Miji) na Halmashauri ya Wilaya Njombe
(Wilaya).
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika
maadhimisho hayo. Kushoto ni Msema Chochote (MC) machachari ambaye pia
ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang'a.
MC
Machachari ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang'a
akisherehesha mambo kwa ufasaha kabisa. Nyuma yake ni kundi la taarab
la TOT ambalo limekuwa likinogesha sherehe hizo.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta na Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Galikunga wakijadili jambo katika maadhimisho
hayo. Hawa ndio viongozi wakuu wa Wilaya ya Nkasi na wenyeji wa
maadhimisho ya siku hiyo ya mazingira kitaifa mwaka huu 2013.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa
akicheza muziki na kundi la Tanzania One Theatre (TOT) waliokuwepo
kutumbuiza katika maadhimisho hayo. TOT wakiongozwa na muimbaji wao
mahiri Khadija Kopa "Heshima Pesa Shkamoo Makelele".....
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakiwa katika banda lao la maonesho.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia