Wabunge wa Chadema, Mh Lema, Mh John Mnyika, Mh Mashishanga, Mh Tundu
Lissu na Grace Kiwhelu wakiwa wamebeba jenenza leneye mwili wa marehemu
Judith William Moshi kuelekea makaburi ya Sokoni 1 kwa maziko. Marehemu
Judith alifikwa na mauti baada ya kulipukiwa na bomu siku ya Mkutano wa
Chadema kuhitimisha kampeni zake kwa udiwani wa Kata ya Kaloleni,
mkutano uliofanyika uwanja wa Soweto siku ya Jumamosi Juni 15, 2013.
Wabunge wengi wa Chadema walishiriki ibada na kuhudhuria mazishi
wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho taifa Mh Freeman Mbowe.
wakiwa wanawasili kwenye msiba kanisani
Wabunge
wa Chadema, Mh Lema, Mh John Mnyika, Mh Mashishanga, Mh Tundu Lissu na
Grace Kiwhelu wakiwa wamebeba jenenza leneye mwili wa marehemu Judith
William Moshi kuelekea makaburi ya Sokoni 1 kwa maziko. Marehemu Judith
alifikwa na mauti baada ya kulipukiwa na bomu siku ya Mkutano wa Chadema
kuhitimisha kampeni zake kwa udiwani wa Kata ya Kaloleni, mkutano
uliofanyika uwanja wa Soweto siku ya Jumamosi Juni 15, 2013. Wabunge
wengi wa Chadema walishiriki ibada na kuhudhuria mazishi wakiongozwa na
mwenyekiti wa chama hicho taifa Mh Freeman Mbowe.
Misa katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Sokon 1
Msafara
wa kwenda Makaburini ukiongozwa na Askofu Isaac Kasir katka Kanisa la
KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Sokoni 1
Jeneza likiteremshwa kaburini
Mh Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” wakiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu
Mtoto wa marehemu akilia kwa uchungu sana baada ya kuweka shada la maua. Marehemu Judith ameacha watoto watatu wote wa kike
Msafara
wa wafuasi wa Chadema ukitoka Hospitali ya Mt Meru kuelekea Kata ya
Sokoni 1 ambako ndipo misa ya kumuombea marehemu na maziko ya Judith
Moshi aliyekufa kwakulipuliwa na bomu Jumamosi iliyopita ilifanyika
Msafara ukikatiaza mitaa ya Jiji kiasi cha kusimamisha shughuli zote katika njia ilikopitia
Hapa ni Sugu akiwa na Peter Msigwa wakiongoza msafara.
Hili ndilo jeneza lililolobeba mwili wa marehemu ukipelekwa Sokon 1
Vijana
walioko kwenye mafunzo ya upolisi wakiwa juu ya kanisa linaloendelea
kujengwa wakati wa ibada ya kumuombea marehemu Judith William Moshi.
Chadema inawatuhumu Polisi ndio waliolipua bomu na kupiga risasi
zilizoua 4 na kujeruhi zaidi ya 67 katika mkutano wake