Mkutano mkuu
wa kijiji cha Salanka umeamua kumsimamisha mtendaji wa kijiji hicho kupisha
uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha za kijiji hicho kutokana na kutotoa
ushirikiano kwa viongozi wa kijiji hicho juu ya upotevu wa pesa za malipo ya kampuni
ya mawasiliano ya simu za mkononi ya(VODACOM)hali iliyopelekea kuwagawa wananchi.
Aidha kwenye
mkutano huo agenda ilikuwa kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha zitokanazo
na minara ya kampuni za simu za Vodacom na Airtel zilizoweka minara ya
mawasiliano kwenye kijiji hicho.
Akifungua
mkutano huo mwenyekiti wa kijiji cha Salanka Hamis Majaliwa alisema kuwa uwazi
kwenye mapato ya jamii unahitajika kwani fedha za umma si mali ya mtu mmoja na
wao wapo kuwatumikia wananchi bila kujali itikadi za kisiasa.
Majaliwa
akafungua mkutano kwa kuwataka wananchi na wakazi wa Salanka kutoa maoni na
ushauri katika kuendeleza gurudumu la maendeleo huku akiwaomba kutokuwa na
jazba kwenye kujadili hatma ya maisha yao kwa utashi wa kisiasa ambao ulianza
kujitokeza katika mkutano huo.
“Nawaombeni
ndugu zangu kuweka itikadi za vyma vyetu pembeni tujadili mustakabali wa maisha
yetu na sanjari na kijiji chetu kwa faida ya vizazi vijavyo”alisema Majaliwa.
Ndipo ikaja
Agenda ya malipo ya minara hapa wakazi hao waliutaka uongozi kutoa mchanganuo
na vielelezo vyote vya malipo ya makampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi
yaliowekeza kijijini hapo hatua ambayo ilimuweka katika wakati mgumu mtendaji
wa kijiji kwani malipo ya kampuni mmojawapo ya Vodacom hayakuwaridhisha
wanakijiji kutokana na kutokuwa na vielelezo vya malipo ya mwaka moja wa
2011-12.
Hali
iliopelekea kwa pamoja kuadhimia kumsimamisha mtendaji wa kijiji hicho na
kumpelekea taarifa mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Kondoa huku wakiitaka
kutuma wakaguzi wa mahesabu ya ndani wa halmashauri hiyo kwenda kuhakiki
mahesabu ya kijiji na kuwa akabidhi ofisi kwa mtendaji wa kata ya Salanka jambo
lililopingwa na mtendaji wa kata hiyo.
Mwandishi
alijaribu kumtafuta mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kondoa kwa simu ya
mkononi namba iliita bila ya kupokelewa na juhudi zaidi zinaendelea ilikupata
ufafanuzi wa sakata hili linaloweza kuchukuwa sura tofauti na yasasa kama
uongozi wa juu hautachukuwa hatua za haraka.
“Uchunguzi
uliofanywa na mwanahabari unaonyesha kuna mapungufu mengi ya kiutendaji na kiuongozi
kati ya mwenyekiti na mtendaji wa kijiji kwa kila mmoja kutokujua mipaka ya
majukumu yake hali inayopelekea kuwagawa wananchi na kukwamisha shughuli za
maendeleo jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa maendeleo ya kijiji.
Kwa upande
mwingine ni ufinyu wa malipo yanayotolewa na makampuni hayo kwa ajili ya
maendeleo ya kijiji hicho hayalingani na malipo wanayofanya kwa sehemu nyingine
walizowekeza minara ya mawasiliano hali inayoashiria kuna harufu ya rushwa kati
ya mtendaji wa kijiji na wawakilishi wa Kampuni ya Vodacom inayolalamikiwa sana
kwenye kadhia hiyo na wakazi wa kijiji hicho.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia