Ticker

6/recent/ticker-posts

BILAL ATEMBELEA MAJERUHI WA BOMU LILILORUSHWA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA


Serekali imewapeleka nchini Kenya Vijana wawili wahanga wa mlipuko wa
mabomu kwenda kupatiwa matibabu zaidi baada ya hali zao kuwa mbaya
kwenye hospital ya Agakhan ya jijini Nairobi.

Akizungumza  na waandishi wa habari mkuu wa mkoa waArusha Magessa

Mulongo alisema kuwa kutokana na maombi ya mama wa watoto hao na
kujali wananchi wake serekali imeamua kuwapeleka watoto Sharifa na
Fatuma Jumanne nchini Kenya kwa matibabu zaidi.

Mulongo alisema kuwa kutokana na ripoti ya madaktari wa hospitali ya

Selian na hali za vijana hao serekali imeamua kugharamia matibabu ya
vijana hao ambaoa wamapata hali mbaya kwenye viungo vyao vya mwili na
Kichwa.

Alisema kuwa timu ya madaktari wa mifupa kutoka Hospitali ya Muhimbili

kitengo cha (MOI)teyari wapo jijini hapa kuungana na madaktari wa
hospitali za selian na hospital ya mkoa Mount Meru kuendelea na
matibabu ya wahanga hao.

“Serekali imeamua kwa dhati kuendelea kutoa msaada kwa wahanga ili

kuweza kuwatibu wote waliopata majeraha kwenye kadhia hii ya bomu na
kuwa wapo pamoja katika kila hali kuhakikisha wanapona kwa gharama
yeyote”alisema Mulongo.

Wakati huo huo Viongozi wa kitaifa akiwemo waziri mkuu yupo njiani

kuja jijini hapa kuendelea kuwapa na kuwafariji wafiwa na wahanga wa
bomu lililotupwa kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha demokrasia na
maendeleo(CHADEMA)wakati wakifunga kampeni ya uchaguzi mdogo wa
udiwani kwenye kata ya Kaloleni jijini hapa juzi.
WAKATI HUO HUO

Serekali imesema kuwa itafanya  kila jitihada kuhakikisha  kuwa wale
ambao wamehusika na tukio la ulipuaji wa bomu  uliotokea katika
mkutano wa kufunga kampeni wa chadema  watatiwa mbarano na kuchukuliwa
hatua kali za kisheria.

Hayo yamebainishwa na makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa

Tanzania  Dkt.Mohammed Gharib Bilal wakati alipowatembelea wahanga wa
bomu lililorushwa June 15 mwaka huu katika mkutano wa chadema .

Alisema kuwa  serekali imepokea kwa masikitiko makubwa jambo hili

ambalo ni la kigaidi na hatasita kumchukulia mtu yeyote aliyehusika na
tukio hili hatua kali za kisheria iwapo atakamatwa .
Aliwataka wananchi wavute subira,wawe wastamilivu  na pia wavumilivu
haswa katika kipindi hichi ambacho upelelezi unaendelea na wasikate
tamaa hata kama itachukuwa muda mrefu.

"napenda kuwaambia msikate tamaa  vuteni subra kwani  aliyehusika

atakamatwa tu hata kama ikitumia muda wa siku tatu ,siku kumi mwezi na
hata miaka mitatu na zaidi lakini aliyefanya tukio hili atakamatwa tu
ata akienda wapi nanachopenda kuwaambia wananchi kuwa mjenge imani na
serekali yanu ya jamuhuri ya muungano wa tanzania na mshirikiane nao
na mwishowe matatizo haya yatakwisha"alisema Bilal

Aidha aliwataka wananchi wajenge imani na mapenzi mema na makubwa kwa

nchi yao na hiyo tu ndo itawasaidia kuwavusha katika katika matatizo
haya ambayo yanatokea kwa kwa kipindi hichi huku akiwasisitiza kuwa
iwapo watajenga imani na mapenzi na serekali yao basi nchi yetu
itakuwa na amani kama zamani na historia yake itaendelea kubaki kuwa
Tanzania ni nchi ya amani .
"pia napenda kuwaambia kuwa tusikubali mtu atuvuruge sisi watanzania
kwani nchi yetu inasifiwa kila kona kwa kuwa na amani hivyo tunapaswa
tuakikishe kuwa tunaendelea kudumisha amani yetu sisi wananchi pamoja
na nchi yetu kwa ujuma.

Aliwapa pole wananchi wate wa mkoa wa Arusha kwa tatizo hili pamoja na

majeruhi wote ambao wameathiriwa na tatizo hili pamoja na wale wote
ambao wamepoteza ndugu zao kutokana na tatizo hili huku akiwashukuru
madaktari wote wale ambao wamewasiadia kuwaguza wagonjwa hawa na
kuwasihi waendelee kuwaudumia vyema hadi pale ambapo watapona .

kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa mulongo alisema kuwa

mpaka kufikia leo asubui idadi ya marehemu imeongezeka na kufikia
watatu  ambapo kijana mmoja ambaye akumtaja jina mwenye umri wa miaka
saba alifariki dunia leo asubui.

Post a Comment

0 Comments