Uwanja wa Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za
kuwania Udiwani Kata ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika
umegeuka kuwa uwanja wa vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka
na kuua watu watatu na zaidi ya 15 kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao
wakiwa wamevunjika miguu.
Katika Mkutano huo walikuwapo pia
Mwenyekiti wa Chadema naa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema
sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati
nzuri Mbowe na Lema ambao walokuwa vinara katika Mkutano huo
hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.
Mlipuko huo ulitokea
mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara baada tu ya Mh
Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka chini na
kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu, hali
inayoashiria mrushaji huenda lilenga kuwajeruhi viongozi hao.
Miili
ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini
hawakupokelewa baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya
wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuwawa.
Baadhi
ya majeruhi ni viongozi wa Chadema ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa wa
Arusha, sambamba na wananchi wa kawaida wakiwemo watoto waliofika
mkutanoni hapo.
Mkutano wa leo ulivunja rekodi ya mahudhurio
viwanjani hapo.. lakini ulikuja kuharibika baada ya kutokea mlipuko huo
haotuba zikiwa zimeishamalizika na baadhi ya watu wakiwa wanatawanyika
kuelekea majumbani huku zoezi la kuchangisha pesa likiendelea, kitendo
kilichowazuia hata wakusanyaji michango kushindwa kumalizia zoezi hilo…
Hali
ikiwa bado tete viwanjani hapo, magari kadhaa ya askari polisi yalifika
huku askari wakiwa na silaha lakini walilazimika kupiga mabomu ya
machozi kadhaa hewani na kisha kuondoka kutokana na baadhi ya wananchi
waliokuwa na hasira kuwafuata na kupaza sauti wakitaka wawaue pia.
Kijana
mmoja muuza machungwa aliieleza blogu hii kuwa aliyerusha bomu hilo
alitokea upande wa nyuma ya jukwaa kuu na badae kukimbilia nyumba
zilizojirani. |