Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu (katikati), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kulia) na Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe ya siku ya wanachama wastaafu (Pensioners) wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Wastaafu.
Wastaafu wakijiandikishankabla ya kuingia katika ukumbi wa Karimjee leo.
Baadhi ya wastaafu wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk. Makongoro Mahanga.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati wa
sherehe ya siku ya Wanachama wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam leo.. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga na Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume.
Mstaafu wa NSSF, Justina Lyela akitoa ushuhuda wa athari za fao la kujitoa wakatti wa sherehe za wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Mstaafu akichangia wakati wa sherehe hizo.
Dar es Salaam, Tanzania
WASTAAFU nchini wametakiwa kuwa mabalozi wazuri kwa familia
na jamii inayowazunguka, kuelewa faida na hasara ya Fao la Kujitoa,
linalokimbiliwa na wanachama wa Mifuko ya Pensheni kwa Wastaafu, licha ya
ukubwa wa athari zake.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Milton
Mahanga, wakati wa sherehe ya Siku ya Wanachama Wastaafu (Pensioners) wa Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee, jijini.
Mahanga alisema kuwa, Fao la Kujitoa ni changamoto ni
changamoto kubwa inayoikabili mifuko mingi ya pensheni nchini likiwamo NSSF na
kwamba, jamii inapaswa kuepuka kukimbilia kujitoa pale wanapobadilisha ajira
kutoka sehemu moja kwenda nyingine au ajira zao zinapokoma.
“Ni vema wastaafu au wanachama wanaohama au kubadili ajira
zao wakaendelea na kuchangia hata wanapokuwa katika ajira binafsi, kuliko
kukimbilia kujitoa ili kuchukua kilicho chao, ambacho umaliza muda mfupi
baadaye na kuishi maisha ya kuhangaika,” alisema Mahanga.
Mahanga akawahikikishia wastaafu maisha bora baada ya kazi
na kusema kuanzishwa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kumebeba dhima ya
kufanikisha hilo, ambapo kazi zake ni kusimamia mifuko yote ya jamii nchini ili
iweze kutoa huduma bora kwa wanachama wake.
“Hakuna anayeweza kubisha kuwa maendeleo tuliyonayo sasa
nchini yametokana na kazi nzuri ya wastaafu katika sekta ya umma na binafsi na
nguvu zao ndio zimelifikisha hapa taifa kimaendeleo, hivyo kuwathamini wastaafu
ni kujali mchango wao, aliongeza Mahanga.
Aidha, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Cresentius Magori
aliwashukuru wastaafu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuhudhuria sherehe hizo,
huku akiahidi hirika kuendelea na juhudi za kuwaelimisha waajiri ili kila mmoja
ajue wajibu alionao kwa wanachama wake na haki zake katika NSSF.
Magori aliongeza kuwa, nia ya kuwa na siku kama hiyo ni
kuonesha namna ushirikiano baina ya wastaafu na NSSF ulivyo na wigo mpana usio
na mwisho, ambapo hafla za kukutana baina ya pande hizo hizo mara moja kwa
mwaka huzaa awazo endelevu yenye tija kwa kila upande.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia