Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila
---
Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi
aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha
akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.
Katika hukumu iliyosomwa jana jioni, mahakama
imesisitiza kuwa kwa kulazimisha viongozi watoke vyama vya siasa,
Tanzania inawanyima wananchi wake fursa huru ya kushiriki kwenye
uongozi.
Mchungaji Mtikila, ambaye ana historia ndefu ya
kukwaruzana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi, alifungua shauri
mahakama ya Afrika mwaka 2011 baada ya jitihada zake za kupindua
mabadiliko ya kikatiba yaliyofuta ugombea binafsi kugonga mwamba kwenye
mahakama za kitaifa