LULU MBONELA NDIYE MISS REDD'S TANGA 2013
Aliyeshinda nafasi ya pili katika mchuano huo uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Omari Chambo na Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima Dendego ni Like Kipenga huku nafasi ya tatu ikienda kwa Hawa Ramadhani,Hawa Twayb aliyekuwa mshindi wa nne wa tano akiwa Judith Molel.
Washindi hao wamejipatia tiketi ya kushiriki shindano la kumtafuta
mrembo wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini Taji la Miss Talent 2013 lilikwenda kwa Azina Mbaga aliyewashinda washiriki wenzie 12 kwa ucezaji wa ngoma za asili ya Kiafrika.
Katika shindano hilo mshindi wa kwanza alizawadiwa kitita cha sh.500, 000 mshindi wa pili 300,000, mshindi wa tatu 250,000 huku mshindi wanne na tano kila mmoja akipata kitita cha sh.200,000 kila mmoja.
Jopo la majaji katika shindano hilo lilohudhuriwa na mashabiki wengi lililongozwa na Boniface Shelufumo huku wasani walionogesha ni pamoja na Beatrice Nabisha,Fabby Dady,Dr John ,Tunda Man na Afua Suleyman huku wasema chochote wakiwa Sakina Lyoka na fred Mwanjala.
Wengine waliopata vyeti ni kampuni ya Al Hayat,CXC Africa,Redds Original,Mkwabi Enterprises,Clauds Media,Jambo leoLavida loca na Michuzi Media Group na Assenga Oscar.blogspot.com
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia