mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki akiwa anamwelezea waziri mkuu jinsi alivyotekwa na kupigwa
Akielezea
kupigwa kwake, Mbunge Joshua Nassari akizungumza na Mbowe na Nyalandu
hospitalini hapo, alisema alikuwa kwenye kata yake ya uchaguzi lakini
ghafla alizingirwa na watu zaidi ya 30.
Alisema katika kundi pia walikuwamo watu watatu wenye asili ya Kisomali ambao wawili kati yao ni wakazi wa jimbo lake la Arumeru.
“Walinishambulia na kunipiga hali iliyonilazimu kukimbilia kwenye gari langu na kutoa bastola ili kujihami, lakini wakati nakimbia nilizidiwa nguvu na watu hao na kuamua kukimbia sehemu asiyoijua ili kuokoa uhai wangu,” aliongeza Mbunge huyo.
“Hivi siasa kwa kweli tunakwenda pabaya maana mtu anashambuliwa bila sababu, nimeumizwa mimi pamoja na mawakala na viongozi wa Chadema waliokuwa Makuyuni,” alisema.