CHANJO YATOLEWA KWA WATOTO WA MKOA WA MANYARA
Zaidi ya watoto 65,701 wenye umri wa kuanzia miezi sita hadi miaka
mitano wa vijiji 65 vya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara,wanatarajiwa kupatiwa
chanjo ya vitamin A na miezi 12 hadi miaka mitano watapata chanjo ya kuzuia
minyoo.
Watoto hao watapatiwa chanjo hiyo,sehemu tofauti ikiwemo vituo vya
afya na zahanati za Serikali na za binafsi na lengo la chanjo hiyo ni kutokomeza
vifo vya watoto chini ya umri huo ifikapo mwaka 2015.
Mkuu wa wilaya ya Hanang’ Christina Mndeme,akizungumza wakati
akizindua chanjo hiyo juzi kwenye kijiji cha Hirbadaw,alisema jamii inatakiwa
kuwapeleka watoto wao kupata chanzo hiyo ili kudhibiti magonjwa hayo ya watoto.
Mndeme aliitaka jamii kushiriki kikamilifu kwa kuhakikisha watoto
wao wanapatiwa chanjo hiyo na kuepukana na dhana potofu kuwa chanjo hiyo ina
madhara kwa watoto wao.
“Serikali inawapenda sana wananchi wake ndiyo sababu imetumia
fedha nyingi kugharimia chanjo hizi,hivyo msiwasikilize wale wote wanaoeneza
fikra potofu juu ya chanjo hizi ambazo watoto wanapatiwa,” alisema Mndeme.
Alisema wazazi wanaowapeleka watoto wao kwenda kupata chanzo hizo
wanapaswa kuwashawishi wenzao kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hizo katika
vituo vya afya na zahanati zilizo karibu na sehemu wanazoishi.
Watoto wanaotarajiwa kupata chanzo hiyo hapa nchini,ni zaidi ya
202,560 ambapo inadaiwa kuwa watoto zaidi ya 15,000 hupoteza maisha kila mwaka
kutokana na maradhi mbalimbali.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia