Serekali imesema kuwa Tukio
la ulipuaji wa bomu la kutwa kwa mkono kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha
demokrasia na maendeleo(CHADEMA) halikubaliki na sio la kibinadamu ambalo
linaashiria kuvuruga amani.
Kauli hiyo imetolewa na waziri
wa mambo ya ndani dkt.Emanuel Nchimbi wakati alipotembelea na kujionea eneo la
tukio la wahanga wa tukio hilo
la bomu katika hospitali za seliani pamoja na hospitali ya mkoa ya Mounti meru
zilizopo jijini hapa.
Nchimbi Alibainisha kuwa hadi
sasa jumla ya watu waliojeruliwa katika tukio hilo
ni 70 ambapo kati yao
wawili wamepoteza maisha na wengi wawili wapo mahututi katika hospitali ya
seliani wanapoendelea na matibabu huku wengine nane wakiwa wameruhusiwa kurudi
majumbani.
Alisema kuwa wao kama serekali
wamepokea tukio hilo kwa masikitiko makubwa na tukio hilo halikubaliki na sio
la kibinadamu na linania mbaya ya kuvuruga amani na wao kama serekali
wanalilaani kwa nguvu zote.
“Kitendo cha kutupwa kwa bomu
serekali inakilaani na kuwa kitendo hichi kinalaaniwa kwa nguvu zote anawataka
wananchi kuwa watulivu wakati huu na kuimarisha usalama na kuwa watoe taarifa
pale mtakapohisi matukio kama haya”alisema
Nchimbi.
Aidha alisema kuwa jeshi la
polisi limetuma wapelelezi wa mabomu kuja na kuwa upelelezi huo utasimamiwa na
mkuu wa operesheni wa jeshi hilo Poul Chagonja huku akiwataka wananchi kutoa
ushirikiano kwa vyombo vya dola huku upelelezi wa awali ukionyesha kuwa ni bomu
la kutupwa kwa mkono.
Waziri Nchimbi alisema kuwa
upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea na
kusema kuwa serekali itafanyajitihada kubwa kukamilisha upelelezi huo na
kuwataka wananchi kutoa taarifa za kuwezesha kusaidia upelelezi kwenye tukio hilo.
Wakati huo huo huko Monduli
kata ya Makuyuni ambako uchaguzi unaendelea imetaarifiwa kuwa Mbunge wa Arumeru
Joshua Nassari amepata kipigo kutoka kwa mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wa CCM na
kuopoteza jicho hadi hivi sasa amalazwa kwenye Hospitali ya Selian ya jijini
hapa kwa matibabu zaidi.
Taarifa zinadai kuwa mbunge
huyo alipata kipigo hicho na kulikimbia gari lake baada
ya kutoelewana lugha na baadhi ya vijana wa kata hiyo hali iliyopelekea kupata
kipigo hicho.
Hadi hivi sasa anaendelea
kupatiwa matibabu kwenye hospitali ya selian baada ya kukimbizwa hopitali ya
karatu na kupewa rufaa kuja kwenye hospitali ya selian.