MBOWE ,LEMA WAJISALIMISHA POLISI

Mwenyekiti wa CHADEMA  Fremaan Mbowe pamoja na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema leo wamejisalimisha polisi kufatia tamko la jeshi la polisi kusema kuwa linawasaka waheshimiwa hao

akingea na waandish wa habari mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA  Fremaan Mbowe alisema kuwa wao wamejisalimisha kama polisi walivyosema wanawatafuta na walipofika waliandika maelezo ambapo alisema kuwa polisi waliwaita kwa mambo mawili moja likiwa ni kwa kuwaoji kwanini walifanya mkutano pasipokuwa wa halali ambapo alisema kuwa 

"jambo la kufanya mkutano pasipo kuwa halali sio kweli kwani polisi walituruhusu tukafanye mkutano katika sehemu hile lakini kinachotushangaza tumefanya wamekuja kutupiga mabomu nakusema sio wa halali na kuhusiana na ushaidi msimamo wangu upo pale pale tunao ushaidi wa kutosha na tunamjua aliyerusha bomu siku ya jumamosi lakini hatuta utaoa hadi pale Rais atakapo unda tume huru ya majaji ili wafatilie swala hili hao ndo tutawaonyesha ushaidi wetu lakini polisi hatuwezi kuwapa "hii ni kauli ya mbowe
chagonja akiongea na waandishi wa habari
kwa upande wa kamishana wa mafunzo na uperesheni ya kijeshi  Paul Chagonja akiongea na waandishi yeye alisema kuwa wamekuja wamewaoji na kuwaomba ushaidi huo lakini waeshimiwa hawa hawakuwaonyesha ushirikiano 

"mbowe alisema kuwa anaushaidi na hata katika vyombo vya habari ametangaza lakini nacho shangaa tulivyomuuliza hapa amesema kuwa hana ushaidi wowote na wala ajawai kutamka hivyo sasa sisi kwakuwa kasema hivyo nitakaa na makachero wangu na tutaangalia jinsi ya kufanya"alisema chagonja

Aidha alisema kuwa alimuliza mbunge wa Arusha mjini kwanini awali alikuja na kuwasifia polisi baadae akaja kuegeuka na wakati alisema kuwa awezi sema uwongo na akasema yeye anafata mwenyekiti wake anachosema.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post