Uchaguzi wa udiwani kwenye jimbo la Arusha umechukuwa
sura mpya baada ya mgombea wa udiwani wa chama cha wananchi (CUF)kwenye kata ya
Elerai John Gilbert Bayo kuangua kilio jukwaani wakati akinadi sera zake mbele
ya wananchi, wakazi wa kata hiyo na katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Mgombea huyo aliangua kilio hicho baada ya kuwaambia
na kuapa mbele ya wakazi hao wa kata yake kuwa hakuwahi kupokea fedha kiasi cha
50 milion kwa ajili ya kupata muafaka wa meye wa jiji la Arusha kama chama cha
demokrasia na maendeleo wanavyodai na kuwa hata weza kukiuka maadili na
kuwatosa waliomchagua.
Akizungumza kwenye kampeni hizo katibu mkuu wa CUF na
makam wa kwanza wa serekali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar Seif Sharif Hamad
aliwataka wakazi wa kata ya Elerai kuwachagua wagombea wa chama hicho kwani
chama hicho kimekuwa kikihimiza umoja na Amani wakti wote.
Maalimu Seifu akabainisha kuwa Mgombea wa CUF kwenye
kata ya Elerai John Bayo ni mtu makini na mchapakazi na kuwa wao hawapo
kumfukuza mtu bali wananchi ndio watakao amua hatma ya viongozi wanaowataka
kwani sisi CUF ndio walimu wa amani hapa nchini kama tungekuwa hatuhubiri amani
Zanzibar isinge kalika baada ya uchaguzi mkuu kwani chaguzi zote tuliweza
kushinda lakini tulipokwa ushindi.
“Sisi CUF ndio wahubiri wa amani kwani tangu mwaka
1995 tumeshinda chaguzi zote lakini kwa hekima na busara tuliwakataza vijana
kuingia barabarani kudai haki yao lakini leo matunda ya busara si mnayaona”alisema
Maalimu Seifu.
Zanzibar wananchi waliishi kwa uhasama na tukaona kama
tutaenda hivyo kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 basi kutaweza kutokea mchafuko
hivyo mimi na Rais mstaafu Karume tulikaa na baaadae vyama na hatimaye wananchi
zaidi ya 66%akaidhinisha muafaka huu ni uamuzi wa busara na leo ndiyo iliyozaa
serekali ya umoja wa kitaifa.
Maalimu akatanabaisha kuwa CUF inaimani na John Bayo
kwa kuwa ndiyo chaguo la wananchi wa kata hiyo na kuwataka kumpa kura zote
iliawe diwani wao na kusema hivi sasa Zanzibar imetulia baada ya mwafaka ule na
haya ni matunda ya chama hicho na kuwa hawatajuta kuchagua mgombea wa chama
hicho kwenye kata zote waliosuimamisha wagombea.
Naye mgombea wa udiwani wa Kata ya Elerai John Bayo
alisema kuwa akichaguliwa atapambana na kero mbalimbali zinazowakabili wakazi
wa kata hiyo ikiwemo kutoa michango ya kununua madawati na majembe kila mwaka
kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Bayo akawataka wakazi wa kata hiyo kuwaonyesha kuwa
hakuchaguliwa na mafuriko ya chadema kwa kumpigia kura ya ndiyo kwenye uchaguzi
huo siku ya tarehe 16 mwezi huu na kuwa majengo ya Zahanati wao hawataki
zahanati bali kituo cha Afya hivyo wakimpa ridhaa hizo zitakuwa kipaumbele
chake