Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WENGI HAWANA ELIMU YA URAIA

 
Mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoani Arusha,Mary Lugola akitoa
semina ya elimu ya uraia iliyoandaliwa na taasisi ya Mategemeo Women
Association ya jijini Arusha(picha na woinde shizza,arusha


 huo




  Katibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Mategemeo Women
Association,Viola Lindikikok
 akitoa mada katika mdahalo wa elimu ya uraia ulioandaliwa na asasi
hiyo na kuwashirikisha zaidi ya vijana 100 kutoka katika kata za
lemara na Daraja mbili za jijini Arusha,pembeni yake ni wahamasishaji
katika mdahalo

Imeelezwa ya kwamba vijana wengi nchini hawana uelewa wa elimu ya uraia hali ambayo imepelekea baadhi yao kushindwa kutambua majukumu yao ya msingi na fursa mbalimbali za kuwaingiza kipato.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na katibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Mategemeo Women Association,Viola Likindikok  wakati alipokuwa akizungumza katika mdahalo wa elimu ya uraia ulioandaliwa na asasi hiyo .

Mdahalo huo uliwashirikisha zaidi ya vijana 100 kutoka kata za Lemara na Daraja mbili ambapo miongoni mwao ni wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo ndani ya kata hizo.

Katibu huyo alisema kwamba katika utafiti wao wamebaini ya kwamba vijana wengi nchini hawana elimu ya kutosha kuhusu suala la uraia hali ambayo imekuwa ikichangia kushindwa kujitambua.

Hatahivyo,alisisitiza ya kuwa  katika midahalo mbalimbali waliyoifanya vijana wengi wamekuwa wakihoji kuhusu suala la ajira ambalo alikiri ni changamoto kuu kwa serikali na kila mdau wa maendeleo  hapa nchini.

Naye,mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoani Arusha,Mary Lugola alisema ni vyema vijana nchini wakapewa elimu ya uraia ili waweze kujitambua na kuepuka kutumiwa katika harakati mbalimbali za kichochezi.

Baadhi ya watoa mada katika mkutano huo,Happy Mwajunga na Salmin Sulle walisema kuwa waliwataka vijana kuacha kulalamika na kukata tamaa katika maisha huku wakiwasisitiza kuwa wadadisi ili waweze kutambua fursa mbalimbali za kuwaingizia kipato.

Post a Comment

0 Comments