Zaidi ya wadau 40 wa sekta ya
fedha kutoka nchi nane za jumuiya ya madola wanapatiwa mafunzo ya teknolojia
mpya ya udhibiti na ukopaji wa madeni ya nje ili kuweza kuthibiti madeni na
ukopaji kwenye nchi zao.
Semina hiyo ya wiki mbili
pamoja na hayo pia watabadilishana uzowefu katika nyanja za kifedha kutoka
kwenye mataifa yalioendelea na nchi zinazoendelea inayofanyika kwenye jiji la Imeelezwa ya kwamba vijana wengi nchini hawana uelewa
wa elimu ya uraia hali ambayo imepelekea baadhi yao
kushindwa kutambua majukumu yao
ya msingi na fursa mbalimbali za kuwaingiza kipato.
Hayo yalisemwa hivi
karibuni na katibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Mategemeo Women
Association,Viola Likindikok wakati alipokuwa akizungumza katika mdahalo
wa elimu ya uraia ulioandaliwa na asasi hiyo .
Mdahalo huo
uliwashirikisha zaidi ya vijana 100 kutoka kata za Lemara na Daraja mbili
ambapo miongoni mwao ni wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo ndani ya kata
hizo.
Katibu huyo alisema kwamba
katika utafiti wao wamebaini ya kwamba vijana wengi nchini hawana elimu ya
kutosha kuhusu suala la uraia hali ambayo imekuwa ikichangia kushindwa kujitambua.
Hatahivyo,alisisitiza ya
kuwa katika midahalo mbalimbali waliyoifanya vijana wengi wamekuwa
wakihoji kuhusu suala la ajira ambalo alikiri ni changamoto kuu kwa serikali na
kila mdau wa maendeleo hapa nchini.
Naye,mkuu wa kitengo cha
polisi jamii mkoani Arusha,Mary Lugola alisema ni vyema vijana nchini wakapewa
elimu ya uraia ili waweze kujitambua na kuepuka kutumiwa katika harakati
mbalimbali za kichochezi.
Baadhi ya watoa mada
katika mkutano huo,Happy Mwajunga na Salmin Sulle walisema kuwa waliwataka
vijana kuacha kulalamika na kukata tamaa katika maisha huku wakiwasisitiza kuwa
wadadisi ili waweze kutambua fursa mbalimbali za kuwaingizia kipato.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia