HII NDO RATIBA YA ZIARA YA OBAMA
Rais Barack Obama.
Ikulu
ya Marekani na Idara ya Habari (Maelezo), wametangaza ratiba ya Rais
Barrack Obama atakapozuru Tanzania huku ikionyesha kuwa atakaa siku
mbili tu, kuanzia Julai Mosi na kuondoka kesho yake.
Tanzania
itakuwa nchi ya mwisho ya Afrika kutembelewa na Obama baada ya Senegal
na Afrika Kusini. Mara atakapowasili na ndege yake kubwa ya Air Force
One, Rais Obama atazindua barabara mpya katika upande wa Mashariki wa
geti la kuingia Ikulu.
Rais Obama, ambaye atafuatana mkewe
Michelle pia siku hiyohiyo atazungumza kwa nyakati tofauti na
wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika na Marekani kwenye Hoteli ya Hyatt
Regency, Dar es Salaam.
“Pia amepanga kuzungumza na maofisa wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,” ilisema taarifa ya Maelezo.
Baada
ya shughuli hiyo, Rais Obama atahudhuria dhifa ya taifa atakayoandaliwa
Ikulu na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete. Siku itakayofuata ataweka
shada la maua kwenye sehemu ulipokuwa Ubalozi wa Marekani ikiwa ni
kumbukumbu ya watu waliofariki katika shambulizi la bomu mwaka 1998. Pia
atatembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion na atatoa
hotuba akizungumzia mikakati ya Marekani ya kulisaidia Bara la Afrika
kuzalisha nishati ya umeme.
“Tanzania ni mshirika muhimu wa
Marekani,” alisema Ofisa wa Ikulu ya Marekani, Ben Rhodes wakati
alipozungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki katika Ikulu ya
Marekani kuhusu ratiba ya ziara ya Obama barani Afrika.
Pia mke
wa Obama atakuwa na ratiba yake. Julai Mosi, atapata staftahi na
mwenyeji wake, Salma Kikwete katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (Wama), Dar es Salaam.
Pia atatembelea sehemu ubalozi
wa zamani wa Marekani na baadaye atashuhudia onyesho la utamaduni la
Kikundi cha Baba wa Watoto, ambacho kinajumuisha watoto wa mitaani wenye
umri kuanzia miaka mitano hadi 18 kwenye Makumbusho ya Taifa. Julai 2,
atahudhuria mkutano na wake wa marais wa nchi za Afrika ambao pia
utahudhuriwa na mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush, Laura
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia