TAARIFA YA JESHI LA POLISI LAMBANA JOYCE KIRIA .... HII HAPA NDIO KAULI YAO
JOYCE KIRIA AKIWA NA MABONGO HUKU AMEBEBA WATOTO WAKE
Joyce Kiria akiwa amebeba mtoto wake
MUME wa joyce kiria Kamanda
Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na watuhumiwa wenzake wanne
wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena
Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013
Na Josephat Isango wa Tanzania Daima
KAIMU
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Dar es
Salaam, Henry Kilewo, anashikiliwa na polisi , akihusishwa na tukio la
kumwagiwa tindikali, Musa Tesha.
Tesha
alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana Septemba 9, mwaka juzi
kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, uliomuweka
madarakani Dk. Kafumu Dalali.
Akizungumza
juzi na Tanzania Daima kabla ya kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi,
Kilewo alisema hajui anachoitiwa na kwamba anatekeleza wito wa jeshi
hilo kuwa afike ofisini kwao.
“Sijui
ninachoitiwa, nimepigiwa simu naenda kutekeleza wito, nimesha wataarifu
mawakili wangu ninaowaamini, kwa kuwa chochote kinaweza kutokea cha
msingi Watanzania wapenda mageuzi waniombee kwa Mungu,” alisema Kilewo.
Wakili
wa Kilewo, Peter Kibatala, alisema baada ya mteja wake kuhojiwa kwa
muda wa saa tano juzi alielezwa kuwa anapelekwa Igunga, mkoani Tabora
kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya kutumia tindikali na
kujeruhi.
Kibatala
alisema anasikitishwa na hatua ya jeshi hilo kumnyima dhamana mteja
wake ilhali kosa wanalomtuhumu linadhaminika na kwamba hayo ni matumizi
mabaya ya madaraka kumzuia mtu kwa zaidi ya saa 24 pasipo kumfikisha
mahakamani.
Wengine
wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutumia tindikali na
kudhuru watu ni pamoja na Oscar Kaijage wa Shinyanga na Evodius
Justinian wa Bukoba.
Evodius
Justinian alikamatwa na Jeshi la Polisi mjini Bukoba na kushikiliwa
kwa siku kadhaa kabla ya kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam.
Kabla
ya kusafirishwa na kufikishwa jijini Da r es Salaam, Justinian alieleza
kuteswa na kupigwa na askari waliokuwa wakimzuia katika vituo
mbalimbali kuanzia mjini Bukoba.


0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia