RATIBA YA MAPOKEZI YA MWILI WA ALBERT MANGWEA HIYO HII.
bywoinde-
0
Tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa watanzania wenzetu kwa
ushirikiano wenu katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa ndugu yetu
Albert Mangweha kilichotokea Afrika Kusini.
Katika kufanikisha
msiba na mazishi ya ndugu yetu mpendwa tunapenda kuchukua nafasi hii
kukaribisha wizara husika, mashirika, makampuni na watu binafsi kutoa
michango yenu kupitia mitandao ya simu zifuatazo:
Kwa watumiaji
wa mtandao Tigo, Nenda kwenye kutoa pesa toa kiasi unachotaka kuchangia
, kisha andika namba ya wakala 00001 ,ambapo litatokea jina la Mangwair
Contribution hapo utakuwa tayari umechangia.
Tigo: Namna ya kuchangia, Nenda kwenye kutoa pesa , andika namba ya
wakala ambayo ni 00001, chagua kiasi unachotaka kuchangia, Jina
litakalokuja ni Mangwair Contribution baada ya hapo utakuwa umechangia. - Mpesa – 0754-967738
Pia kwa kutumia akaunti ya benki ifuatayo: - Jina la Akaunti : Kenneth B. Mangweha Nambari ya Akaunti: 2012505840 Benki : NMB Pia kwa niaba ya kamati tunapenda kutoa ratiba kama ifuatavyo:
Mwili wa marehemu utafika siku ya jumamosi tarehe 01/06/2013 saa 8
adhuhuri katika kiwanja cha Jk Nyerere na kupelekwa hospitali ya
Muhimbili.
SIku ya Jumapili tarehe 02/06/2013, tunapenda
kuwakaribisha watanzania wenzetu katika viwanja vya Leaders kwa ajili ya
kuaga mwili wa marehemu. Shughuli itakayoanza saa 2 ya asubuhi mpaka
saa 6 mchana.
Saa 6 mchana Mwili wa marehemu utaondoka kuelekea Morogoro kwa ajili ya maziko yatayofanyika siku ya jumatatu.
Siku ya jumnne tarehe 04/06/2013, mwili ya marehemu utafika saa 8
asubuhi nyumbani kwa mama yake maeneo ya Kihonda mjini Morogoro saa sita
kutakuwa na chakula na baada ya hapo tutaaga mwili wa marehemu kwa
ajili ya Maziko.
Tukiamini kila mwenye uwezo atachangia katika kufanikisha shughuli hii tunatanguliza shukurani zetu za dhati.
Pia tunaomba watanzania mujitokeze kwa wingi katika kuaga mwili wa
marehemu katika kuonyesha upendo wetu kwa ndugu yetu Albert Mangweha.