HALI YA RAIS MSTAAFU SOUTH AFRIKA NELSON MANDELA YAZIDI KUWA MBAYA HOFU YATANDA DUNIA NZIMA
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ikulu ya nchi hiyo mjini Pretoria zilisema mpaka kufikia leo jioni Mandela alikuwa amezidiwa ingawa madaktari wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa anapata afueni, ingawa ikulu iliwahakikishia wananchi kuwa wasiwe wasiwasi sana.
Mandela ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, akiwa na umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema mwezi huu, ikiwa ni mara ya tatu kwake kulazwa hospitalini akiugua ugonjwa wa mapafu mwaka huu.
Rais Jacob Zuma alisema Jumapili kuwa alimzuru Mandela Hospitalini na kuzungumza na mkewe kuhusu hali ya rais mstaafu.
Madaktari wanaomtibu Mzee Nelson Mandela walimwambia Rais Zuma kuwa hali ya Mandela imekuwa sio nzuri kwa saa zaidi ya ishirini na nne zilizopita na yupo mahututi.
Nje ya hospitali alikolazwa Mandela, watu wamekuwa katika hali ya utulivu huku wanafamilia wake wakirejea toka sehemu mbalimbali duniani. Kuta za hozpitali hiyo zimeonekana kupambwa na kadi nyingi na maua ya kumtakia heri, na kupona haraka Rais huyo wa zamani.
Ailing: President Jacob Zuma places a hand on Mr Mandela's, whose head was supported by a pillow and knees covered by a blanket following his release from hospital in April
Rais Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela na pia kuzungumza na jopo la matabibu wanaomtibu. Zuma alirejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumuombea Mzee Mandela apate nafuu.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia