KILIMANJARO
mwalimu mkuu wa shule ya msingi iliyopo wilayani Rombo Mkoani
Kilimanjaro (jina tunalihifadhi) anatuhumiwa kumtia mimba mwanafunzi wa
shule ya sekondari ya Boon, mwenye umri wa miaka 17.
Mwalimu huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kiusalama
alimpa ujauzito binti huyo na kupelekea uongozi wa shule hiyo kumfukuza
shule kwa mujibu wa kanuni na sheria za kiserikali.
Akizungumza na mwanaharakati wa mtandao huu wa Kilimanjaro Official Blog jana katika mahojiano maalumu
Mkuu wa shule ya sekeondari ya Boon anaposoma binti huyo aliyepewa uja
uzito. Mwalimu mkuu huyo alikiri kweli mwanafunzi huyo ni mjamzito na
mimba hiyo ni ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi iliyopo wilayani Rombo.
Shirima alisema mwanafunzi huyo alibainika akiwa na jauzito huo Novemba
25 mwaka huu baada ya ugomvi mkubwa kuzuka shuleni hapo baina ya
mwanafunzi huyo na mwanafunzi mwingine wakimgombea mwalimu mkuu huyo
aliyempa ujauzito.
Alisema baada ya ugomvi huo ndipo mwanafunzi mmoja alitoka na kwenda kwa
mwalimu wa malenzi na kumweleza suala hilo na ndipo uongozi wa shule
ulichukua hatua ya kwenda na kumpima binti huyo ambapo alibainika
anaujauzito wa mienzi nne.
Alisema baada ya vipimo kuthibitisha mwanafunzi huyo ni mjamzito uongozi
wa shule hiyo ulitoa taarifa katika kituo cha polisi Mengwe na jambo
lililofanikisha mwalimu huyo kushikiliwa kwa maojiano zaidi.
Aidha alisema baada ya hatua hiyo alitoa taarifa pia kwa mtendaji wa
kijiji na diwani wa kata hiyo ambapo wazazi wake walitaarifiwa na
kukabidhiwa mtoto wao mbele ya viongozi hao.
Alisema changamoto kubwa inayo wakabili ni wazazi kufanya siri na
kuficha matukio hayo pamoja na jitihada zinazofanyika katika kutokomeza
mimba mashuleni.
Mwalimu huyo alisema tukio hilo ni tukio la pili la walimu kuwapa mimba
wanafunzi na kwamba wamekuwa wakisikitishwa na hatua zinazochukuliwa
kutokana na mmoja wa mwalimu aliyetenda kosa hilo kuendelea kufundisha
na kuzurura mitaani na hakuna hatua yeyote aliyochukuliwa dhidi ya kosa
alilotenda la kumpa mwanafunzi ujauzito.
Shirima alisema wazazi wamekuwa wakichangia vitendo vya kuporomoka kwa
maadili ya watoto kutokana na kuwakabidhi simu ambazo wamekuwa
wakiwasiliana na wanaume na kupeleka kupata ujauzito na kupoteza sifa ya
kuendelea na masomo.
Aidha alisema watoto wengi wamekuwa wakiishi na bibi zao hivyo
kushindwa kupata malezi bora kutoka kwa wazazi wao binafsi huku walezi
wengine wakiwa kwenye shuhuli zao za kutafuta pesa na kusau wajibu wa
malezi ya watoto.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia