KATIKA MASHINDANO YA MICHEZO YA MABUNGE YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YANAYOENDELEA JIJINI ARUSHA TIMU YA BUNGE LA KENYA NA TANZANIA WATOKA BILA BILA
Wachezaji wa Tanzania na Kenya wakiwa katika mashindano ya wabunge wa jumuiya ya Afrika mashariki leo, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume
jijini Arusha, mechi hiyo ilivuta hisia za wakazi wa jiji hilo
waliomiminika kuja kushuhudia wabunge hao wakimenyana uwanjani, baada ya
dakika ya tano bunge la kenya walijipatia bao la kwanza, bao
lililofungwa na Mh.Steven Nyatta na hatimaye Tanzania kusawazisha dakika
ya 24 kwa njia ya penalt baada ya Mh.Mbunge Joshua Nassari kudondoshwa
eneo la hatari kwa kugongwa na mlinda mlango wa kenya Kega Kanin
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mh Iddi Azan mlinda malango
ambaye pia ni kiongozi wa timu ya bunge la Tanzania akinyaka magoli
akionyesha umahiri wake wa kudaka mpira hali iliyosababisha mashabiki wa
jiji la Arusha kumshangilia
Mlinda mlango wa Timu ya kenya Kega Kanin akijaribu kuzuia goli lililopatikana kwa njia ya penalt katika dakika ya 24
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akichechemea uwanjani baada ya kuanguka na kupewa huduma ya kwanza
Muonekano jukwaa kuu
Wachezaji wa timu ya Tanzania wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza
Wachezaji wa timu ya Kenya wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza
Kushoto ni mchezaji wa timu ya kenya Mh.Peter
Kaluma katikati ni Mh Dan Wanyama wa kenya mrefu kuliko wote uwanjani
alipewa kadi nyekundu baada ya kuonekana akijibizana na mwamuzi
aliyekuwa akichezesha mpambano huo kulia ni Mh Joshua Nassari wa
Tanzania
Kushoto
Mh Iddi Azan ambaye ni mlinda malango wa timu ya Tanzania akiwa katika
mapumziko, aliyeshikilia mpira ni mwamuzi wa mpambano huo Erick Onoko
Mh Joshua Nassari wa Tanzania akipewa huduma ya kwanza
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akipatiwa huduma ya kwanza
Mh.Mbunge
wa Tanzania akiwa amelala chali akionekana kuwa na maumivu makali baada
ya kuumia katika mechi hiyo wabunge wenzake wakijaribu kumsaidia
Mashabiki wa Kenya wakiwa wanashangilia huku wakiwa wanaonyesha bwebweeee zao
Umati wa watu waliokuja kushuhudia mpambano wa Tanzania na Kenya
Mashabiki wa Tanzania wakiwa wanashangilia kwa kuzunguka uwanja
Watoa huduma ya kwanza kutoka msalaba mwekundu wakiwa wanafatilia mechi ya wabunge wa Afrika mashariki
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia