MABADILIKO YA TABIA NCHI YAWAATHIRI WAFUNGAJI WA NGORONGORO ,LOLIONDO NA MONDULI




WAFUGAJI kutoka  Wilaya za Ngorongoro ,Longido na Monduli wameeleza
kuanza kukumbwa na athari za matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa na
tabia nchi.



Wakizungumza katika  kongamano la jamii  za kifugaji zinazoishi katika
nyanda kame lililoandaliwa na  shirika la  Haki kazi Catalyst   na
taasisi ya kimataifa ya mazingira na maendeleo (IIED)  viongozi wa
jamii hiyo walisema kuwa  tayari wameanza  kukosa mvua za kutosha
katika maeneo yao



" Joto limekuwa kali sana, mvua hazitabiriki ,tunashindwa kujua misimu
tuliyozea,wakati mwingine mvua kubwa inanyesha kiasi cha kuleta hofu
na mafuriko  makubwa tofauti na siku za nyuma ,hali hii ni ishara kuwa
hali ya siku zijazo ni tete"alisema  Martalo.



Diwani wa viti maalum kutoka Wilaya ya Ngorongoro Tina Timan alisema
kuwa  kwa sasa wanawake wa jamii hizo wanasafiri umbali kutafuta maji
kufuatia vyanzo vya maji kukauka kufuatia hali ya ukame.



"Nimefurahi kwa mpango huu na hasa kutokana na kushirikisha wanawake
wa jamii za kifugaji ambao ndio wahanga wakubwa wa tatizo hili ,sisi
ndio tunasafiri mbali kufuata maji ,kutafuta kuni " .anasema Tin

.

Tina aliongeza kuwa migogoro ya ardhi na sera mbalimbali zinawaweka
wafugaji katika hatari zaidi ,maeneo yao yanachukuliwa na kugeuzwa
hifadhi na mengine kupewa wawekezaji tunaomba katika mikakati hii hili
nalo litazamwe.

Esupat Ngulupa kutoka Longido alisema kuwa miaka michache iliyopita
wafugaji walipoteza idadi kubwa ya mifugo baada Wilaya hiyo kukumbwa
na ukame uliodumu  kwa muda mrefu.



"Tunashukuru mashirika haya kujitokeza kutuelimisha namna ya kupambana
athari zitokanazo na mbadiloko ya hali ya hewa na tabia nchi"alisema
Esupat.



Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo kutoka  taasisi ya kimataifa ya
mazingira na maendeleo (IIED)Alais Morindat  alisema  kuwa mafunzo
hayo  yatawasaidia jamii hiyo kuweka mikakati na mipango ya kukabili
athari za mabadiliko ya tabia nchi.



"Kila Wilaya ina mratibu ambaye pamoja na wawakilishi wa jamii katika
Wilaya husika wataweka mipango ya kukabiliana na matokeo ya tatizo
hili'alisema Morindat.,



Alisema kuwa jamii pamoja na viongozi wa kisiasa  ilishiriki
kikamilifu katika kongamano hilo na kutoa mawazo na uzoefu,
kutafakari kwa pamoja sera na dira ya maendeleo ya taifa katika
kuondoa umaskini na jitihada za taifa katika kukabili mabadiliko ya
hali ya hewa na tabia nchi.



Aidha Morindat aliongeza kuwa washiriki pia walijadili kwa undani
masuala ya msingi juu ya dhana na Sayansi ya mabdiliko ya hali ya hewa
na tabia Nchi pamoja na   Mifumo ya wafugaji iliyopo na inayopotea
katika kuhimili mabadiliko mbalimbali yanayotokea.



Sera na sheria za nchi na jinsi inavyowezesha ama kutowezesha mifumo
hiyo ya kijamii kufanya kazi na mabadiliko makubwa ya kiuchumi duniani
faida na athari zake kwa mifumo ya Kijamii.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post