Kiongozi
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe akizungumza kwenye
kikao cha maamuzi ya pamoja na Vyama vingine juu ya kususia mjadala wa
Marerkebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Bungeni juzi jioni.
Kushoto ni Mbunge wa Mkanyageni,Hbib Mnyaa(CUF)na Mbunge wa Kuteuliwa
NCCR Mageuzi, James Mbatia. Picha na Fidelis Felix.
DODOMA.
MAONI ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa 2013 yanadaiwa kuwa yalibadilishwa dakika za mwisho na kwam
ba suala hilo ndicho kiini cha vurugu zilizotokea bungeni mjini Dodoma juzi.
MAONI ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa 2013 yanadaiwa kuwa yalibadilishwa dakika za mwisho na kwam
ba suala hilo ndicho kiini cha vurugu zilizotokea bungeni mjini Dodoma juzi.
Gazeti
hili limefanikiwa kuona nakala inayodaiwa kuwa ni maoni ya awali ya
kamati hiyo ambayo yalikuwa na mapendekezo yanayotaka kuwapo kwa
marekebisho kadhaa kwenye muswada huo, tofauti na yale yaliyowasilishwa
bungeni juzi na Mwenyekiti wa Kamati, Pindi Chana.
Jumatano
na Alhamisi wiki hii kulikuwa na mvutano mkubwa bungeni kiasi cha
wabunge wa upinzani kutoka vyama vitatu vya NCCR -Mageuzi, Chadema na
CUF kuungana na kususia mjadala kuhusu muswada huo.
Imedokezwa
kuwa mvutano mkali kuhusu muswada huo ulianza ndani ya kamati hiyo
wakati wajumbe wake ambao ni wabunge wa CCM walipotumia wingi wao
kubadili maoni ya awali na kuweka maoni mapya, hatua ambayo inadaiwa
kuwa ilikuwa na msukumo wa Serikali nyuma yake.
Ndani
ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, wabunge wa upinzani
ambao kwa idadi yao ni wachache walishindwa kuzuia mabadiliko hayo ya
“lala salama” yanayodaiwa kuwa yaliwekwa Septemba 2, mwaka huu, hivyo
waliazimia kuhamasisha wabunge wote wa upinzani kupinga marekebisho hayo
kutokana na sababu kuu mbili.
Sababu
hizo ni kutofanyika kwa mikutano ya wazi kwa umma (public hearing)
upande wa Zanzibar na hatua ya kuwapo kwa mapendekezo ya Rais
kurundikiwa madaraka makubwa ya uteuzi wa wabunge kutoka asasi za
kijamii watakaoingia katika Bunge la Katiba.
Habari
zinasema wakati fulani Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alitembelea
kamati hiyo wakati ikiedelea na vikao vyake na kukuta mvutano mkali
kuhusu suala la marekebisho ya sheria ya sheria hiyo na alishauri kwamba
pale ambapo hawataweza kuelewana basi wasubiri uamuzi ndani ya Bunge.
Jana
gazeti hili lilimtafuta Chana kupitia simu yake ya mkononi na baada ya
kumweleza kuhusu madai hayo alisema: “Tafadhali sana kwa sasa niko
kwenye kikao, kwanza simu yako nimeipokea kwa heshima tu, tutafutane
wakati mwingine”.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alikiri kwamba kulikuwa na
mapendekezo ya kuongeza idadi ya wabunge na namna ya kuwapata, lakini
Serikali iliyakataa katika hatua ya majadiliano kabla ya suala hilo
kufikishwa bungeni.
Tofauti ya maoni
Nakala
ya taarifa ya awali ilipendekezwa kuwa katika kuteua wajumbe 166 wa
Bunge la Katiba, Rais azingatie kikamilifu mtiririko wa mapendekezo ya
kila kundi lililoainishwa katika kifungu cha (1) (c).
“Na
endapo Rais hatazingatia mapendekezo ya kundi mojawapo, Rais afanye
mrejesho kwa taarifa kwa kundi husika juu ya sababu za kutozingatia
mtiririko wa mapendekezo yaliyowasilishwa kwake,” inasema taarifa
hiyo.MWANANCHI