Marehemu
Neema Malimbwi enzi za uhai wake.
WAKATI Wakristo kote nchini wakijiandaa
kusherehekea Sikukuu ya Krismasi, keshokutwa Alhamisi, baadhi ya
familia zipo kwenye majonzi mazito kufuatia kuondokewa na ndugu zao,
Uwazi lina kisa cha kuumiza.
Jijini
Dar es Salaam, binti mbichi aliyejulikana kwa jina la Neema Malimbwi
(pichani) ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Kodi Tanzania (ITA)
ambacho kipo chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kilichopo
Mikocheni jijini Dar amefariki dunia kwa madai ya kulishwa sumu kwenye
kinywaji.
Marehemu Neema alikuwa binti wa profesa wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro (Sua), Rogers Malimbwi.
SIKU YA TUKIO
Tukio
hilo la kusikitisha linatajwa kutokea usiku wa Alhamisi, Desemba 18,
mwaka huu wakati Neema anarudi hosteli maeneo ya Kijitonyama, Dar ambapo
alikuwa akiishi.
ALIKWENDA KUJIRUSHA B BAND
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, siku ya tukio, Neema alikuwa na marafiki zake
wavulana kwa wasichana kwenye onesho la muziki wa B Band inayomilikiwa
na Banana Zorro ambapo akiwa huko saa 7 usiku aliendelea kuchati na
marafiki zake waliokuwa hosteli akitumia ukurasa wake wa Facebook
akiwaambia kuwa alikuwa ‘kiwanja’ akiponda raha.
Baba wa
marehemu Neema Malimbwi, Prof. Rogers Malimbwi. Habari zinadai kuwa,
marehemu Neema usiku huo alikuwa akihama maeneo mbalimbali akiwa na
vijana ambao baadhi ya marafiki zake wanadai huenda walihusika na
kumtilia sumu kwenye bia alizokuwa akinywa.
MATATIZO YALIPOANZA
Habari zaidi zinasema kuwa, Neema akiwa na wenzake wakirudi hosteli, njiani alianza kulalamikia kutojisikia vizuri.
“Alikuwa
njiani na wenzake wakirudi kulala, akaanza kulalamika kwamba hajisikii
sawasawa, ikabidi wenzake wamkimbize Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu wa
Kinondoni, Palestina, Sinza, Dar ambako waliambiwa kuwa kutokana na hali
yake kuwa mbaya wampeleke kwanza Kituo cha Polisi cha Kijitonyama
‘Mabatini’ jijini Dar ili kupata hati ya matibabu (PF3),” kilisema
chanzo kimoja.Chanzo hicho kikaendelea kudai kwamba, walipofika Mabatini
waliambiwa waende Kituo cha Polisi Oysterbay.
AKIMBIZWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA
Ikazidi
kudaiwa kuwa, Polisi Oysterbay walitoa msaada kwa haraka ambapo sasa
ikabidi Neema akimbizwe Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni,
Mwananyamala ambako alifariki dunia.
CHANZO:UWAZI
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia