WAZIRI wa
Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamanolililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto
wanazozipata wadau hao
waziri wa ajira na kazi Gaudensia Kabaka akiwa katika picha ya pamoja wadau waliouthuria katika konga mano hilo
Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Bg Tanzania Ms Kate Sullam anaemfatia ni Mr Jean Van Wetter ni mkurugenzi wa VSO Tanzania
picha ya pamoja ya washiriki wa kongamono hilo wakiwa pamoja na waziri wa ajira na kazi nje ya ukumbi wa hotel ya Naura Springs iliopo ndani ya jiji la Arusha
waziri kabaka wa kwanza kulia akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa Idrissa Mshoro wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi ayupo pichani kuhusiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta)
WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamano
baadhi ya waandishi wakiendelea kufatilia kwa makini kongamano hilo
washiriki wakifuatilia
washiriki wakiendelea kufuatilia kwa makini
Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi akiwa anaongea katika kongamano hilo
wadau kutoka sekta ya gesi na petrol wakiwa wanafatilia
katibu mkuu wa VET Pro.Sifuni Mchome akiwa anawakilisha mada
Na Woinde Shizza,Arusha
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta)wametakiwa
kuhakikisha wanasikiliza maoni ya wadau ili kujua mahitaji yao sambamba na
kubadili mitaala ya elimu ya mafunzo yanayotolewa kwenye vyuo hivyo ili kuendana na soko la ajira lililopo
hivi sasa.
Hayo yanesemwa leo jijini hapa na WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao na nini chakuongeza kwa vijana wanaopitia Veta na kupata ajira katika sekta mbalimbali sanjari na kuzindua kitabu kinachoanisha mahitaji ya soko la ajira kwa vijana
Aidha aliwataka vijana kutumia fursa za kujiunga na Veta ili waweze kujiariri badala ya
kufanya biashara za kuuza vitu mikononi
bali watumie taaluma walizozipata
kuzalisha vitu vyenye ubora.
Alisema vijana
wanaopitia vyuo vya mafunzo Veta si wengi sana huku wimbi la vijana likiwa bado
mitaani na kuuza bidhaa zao mabarabarani hivyo ni vyema sasa vijana hao
wakaondoka barabarani na kujiunga na vyuo vya ufundi ili waweze kupata mbinu za
kutengeneza vitu sambamba na kupata masoko ya uhakika.
Alisema ni
vyema sasa Vyuo vya Veta vikaweka mkazo katika sekta ya madini na gesi ili
waweze kuangalia mahitaji ya wataalam ni yapi na kutoa elimu hiyo ambayo
itawezesha vijana wengi kupata ajira na kukuza uchumi wan chi.
“Mahitaji ya
vijana ni mengi katika sekta rasmi na zisizo rasmi na kia sekta inamtegemea mtu
fulani hivyo ni vyema Veta mkasikiliza mahitaji ya wadau sambamba na kutafuta
mbinu za kufundisha zaidi ili kuendana na mahitaji ya soko na nyinyi vijana
tokeni barabarani mkajiunge na vyuo vya ufundi ili kuweza kuuza biashara zenu
kwa ubora badala ya kukimbilia kuuza barabarani “.
Naye
Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi alisema kongamano hilo hufanyika
kila mwaka na kushirikisha wadau katika sekta mbalimbali ili kujadili masuala
mbalimbali na mahitaji ya wadau hao katika sekta ya ajira sambamba na kuboresha
mitaala itakayokwenda na wakati na kuwezesha vijana wanaopitia Veta kuwa bora
zaidi kipindi cha kumaliza chuo na kupata ajira.
Alisema pia
Veta inakabiliwa na uhaba wa rasilimali fedha
kwenye ujenzi wa vyuo vipya kwenye Wilaya mpya ambazo ni Katavi, Geita,
Njombe na Simiu lakini pia kuonaongezeko kubwa la vijana na watu mbalimbali
ambao wanajiunga na vyuo hivyo nchini kwaajili ya kupata mafunzo mbalimbali
yanayowawezesha kupata ajira.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa
Idrissa Mshoro alisisitiza kuwa Veta
inatambua na kuthamini maeneo mbalimbali yanayohitaji soko la ajira ndio maana
vijana wanaopata ujuzi kupitia veta wanafanya kazi kwa makini na kujipatia
vipato zaidi.
Aliongeza
kuwa hivi sasa Veta inashirikiana na tasisi na mashirika mbalimbali hususan ya
sekta ya madini na gesi na kutoa mafunzo kwaajili ya kuwasaidia vijana
kukabiliana na soko la ajira .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia