BREAKING NEWS

Saturday, December 6, 2014

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA APANIA KUIREJESHA TIMU YA AFC LIGI KUU




Juma Iddi (mwenye suti nyeusi) ni Mkurugenzi wa jiji la Arusha 
Na Woinde Shizza,Arusha
Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Juma Iddi amepania kuipandisha ligi timu ya Arusha FC inayoshiriki ligi daraja la pili msimu huu, huku akiwataka viongozi wa sasa wa timu hiyo kuwa kama kamati na jiji hilo kuhakikisha swala hilo linafanikiwa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mapema  ofisini kwake alisema kuwa kwa kuwa tayari usajili umekwisha fanyika kwa sasa wanatafuta kocha mwenye ujuzi na uwezo wa kimataifa wa kuwanoa vijana hao ili kuweza kumudu mikiki ya ligi daraja la pili bila kuwa na woga.

“Kiukweli mimi napenda michezo na niko hapa halmashauri ambapo kazi kubwa ni pamoja na kuitangaza michezo na kuonyesha mfano hivyo kwa kuanzia tumeipa nguvu ya kushiriki michuano hiyo kwa vifaa vyote walivyohitaji vya michezo  lengo wasianze kulalama na vifaa”

“Na baada ya vifaa sasa tutahakikisha inakuwa mikononi mwetu mapema mwezi ujao baraza la madiwani litakapokaa na kuridhia na baadhi ya watendaji wa halmashauri hii watakuwa miongozi mwa viongozi watakaochaguliwa kuiongoza lengo ni kuileta karibu na kujua mahitaji yao” alisema Juma Iddi.

Alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa Arusha kuhakikisha wanakuwa karibu zaidi na timu hiyo na ilete chachu ya soka mkoani hapa kwa kuishangilia na mawazo pia maoni yao.

“sisi kama halmashauri kuimiliki timu hii siyo kuwaweka mbali wananchi bali ni kuweza kuwajulisha kuwa pia kuwa timu hiyo ni yao kwani itakuwa inatangaza jiji pia kodi zao ndio zitatumika na wajue kuwa pia hatutachukua moja kwa moja bali kwa mda ili tu kuipandisha”

Alitumia fursa hiyo kuwataka mashabiki wa soka wa mkoani hapa pamoja na benchi la ufundi na wachezaji kuwa kitu kimoja na wasiruhusu migogoro kati yao kwani kufanya hivyo kutakatisha matumaini ya kupanda ligi bali wawe kitu kimoja kuhakikisha lengo linafanikiwa.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates