MADEREVA MBEYA WAFIKIWA NA HUDUMA YA ''WAIT TO SEND''

Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Mbeya Mkunde Said (kushoto)akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Fikiri Sabigo kwa kutumia kifaa maalum wakati wa upimaji madereva ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya”Wait to Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo.Katikati ni Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini Macfadyne Minja Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Mbeya yaendayo mikoani katika mwendelezo wa kampeni hiyo inayofanyika nchi nzima na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Dereva wa mabasi yaendayo mikoani Mohamed Shaban(kushoto)akipimwa kiwango cha pombe mwilini na Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Mbeya,Mapunda Ahmed(kulia)kwa kutumia kifaa maalum wakati wa upimaji madereva ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya”Wait to Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo.Katikati ni Nashon Mudala mtaalam wa usalama na Afya na mazingira wa Vodacom Tanzania.Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Mbeya yaendayo mikoani katika mwendelezo wa kampeni hiyo inayofanyika nchi nzima na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Mbeya Mapunda Ahmed (kulia)akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Simon Mwalugu kwa kutumia kifaa maalum wakati wa upimaji madereva ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya”Wait to Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo.Katikati ni Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini Macfadyne Minja.Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Mbeya yaendayo mikoani katika mwendelezo wa kampeni hiyo inayofanyika nchi nzima na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini Macfadyne Minja(katikati)akimfafanulia jambo kuhusiana na kampeni ya “Wait to Send”dereva wa basi la kwenda mikoani, Simon Mwalugu.Wakati wa zoezi la upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani zoezi hilo lilifanyika leo katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo inayofanyika nchi nzima na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,kulia . Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Mbeya Mapunda Ahmed.

Kampeni ya usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani iliyozinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mathias Chikawe,leo imeendelea mjini Mbeya.

Madereva wameendelea kuhimizwa kutotumia vinywaji vyenye ulevi na kuacha tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Butusyo Mwambelo amesema kampeni hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya ajali “Watumiaji wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto hawana budi kuzingatia maelekezo ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate matokeo mazuri kwa kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema

Alisema madereva wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa ajali zinazoendelea kutokea kila siku zitapunga hususani katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya Krismas na mwaka mpya na aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu.

Kwa upande wake,Mkuu wa kanda ya Nyanda za juu wa Vodacom Tanzania Macfadyne Minja, alisema Vodacom itaendelea kushirikiana na serikali kuunga mkono jitihada za kuondoa matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunaomba madereva kufuata sheria za barabarani kwa usalama wenu,usalama wa abiria mnaowabeba na watumiaji wengine wa barabara".

Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni ya "Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.Mbali na kampeni hii alisema kwa mwaka huu kampuni ilidhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.

Alisema kabla ya uzinduzi wa kampeni ya leo tayari umefanyika uhamasishaji wa madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Dar es Salaam,Mwanza,Arusha na kampeni itaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini Katika kampeni ya leo wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa usalama barabarani na wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabani walitoa uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na simu wanapoendesha vyombo vya moto na kuwagawia madereva pete maalum za kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto pia zoezi la kupima madereva kubaini kama wanatumia vilevi lilifanyika ambapo wadereva waliokutwa wanaendeshwa vyombo vya moto walichukuliwa hatua kali za kisheria.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post