Serikali
Mkoani Arusha Imewataka wakazi wa Mkoa huo Kuhakikisha kuwa wanaendelea
kudumisha Amani,Umoja na Mshikamano sanjari na kujitolea katika kufanikisha
shughuli za kimaendeleo.
Kauli hiyo
imetolewa na katibu Tawala wa mkoa huu Addo Mapunda wakati akiongea na
wanahabari ofisini kwake ambapo alisisitiza
wakazi wa mkoa huu kufuata sheria kanuni
na taratibu za nchi ikwemo usafi wa mazingira.
Aliwatahadharisha
wananchi hao kutofuata mkumbo na kujihusisha na ushabiki wa baadhi ya vyama vya
siasa ambavyo vimekuwa vikiendesha siasa za chuki,udini na uhasama jambo ambalo
limekuwa likiwagawa wananchi katika makundi na kupelekea uwepo wa vitendo vya
uvunjifu wa amani.
“napenda
kuwakukumbusha wananchi wa mkoa wa Arusha kuwa suala la maendeleo sio la
Serikali pekee bali ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa nashiriki
kikamilifu katika shughuli za kujiletea maendeleo”alisema Mapunda.
Akizungumzia
shule za Sekondari za Kata amesema kuwa Serikali imejipanga kikamilifu na
tayari umaliziaji wa majengo ya maabara na vyumba vya madarasa uko katika hatua
za mwisho kabisa kukamilika na kuwataka wananchi kuepukana na dhana potofu kuwa
shule za Kata hazina viwango vizuri vya ufaulu wa wanafunzi.
Mapunda
amesema kuwa Mkoa wake umejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi
hata mmoja aliyechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani ambaye atakosa
kujiunga na shule kwa uhaba wa vyumba vya madarasa kwani mkoa umejipanga
kikamilifu kukabiliana na changamoto hiyo.
Kuhusu suala
la uchaguzi wa serikali za mitaa alisema
kuwa anashukuru uchaguzi huo umekwenda kwa mafanikio na kuwa wananchi walipewa
fursa zxa kuwachaguwa viongozi wanaowataka.
“Kikubwa ni
wananchi kupewa fursa za kuwachagua viongozi
wanowataka bila ya kuwepo
shinikizo hali ambayo imekuwa ikichangia uvunjifu wa Amani ndio maana umeona
mkoa huu hauna matukio ya uvunjifu wa amani kama ilivyokuwa kabla”
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia