Balozi
Ndayiziga katika mojawapo ya warsha ya EAC hivi karibuni. Kulia ni
mtaalamu wa habari na mratibu wa mafunzo ya wandishi wa habari EAC, Bw.
Sukhdev Chhatbar.
Mkufunzi
katika Mafunzo hayo, Balozi Jeremy Ndayiziga (kushoto enzi za uhai
wake) akimkabidhi cheti Mroki Mroki, kutoka Father Kidevu Blog ambaye
pia ni Mpigapicha wa Masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, kwa kushiriki kikamilifu mafunzo hayo ya masuala ya
Mtengamano wa EAC. Anaeshuhudia Katikati ni Elizabeth Wanyoike wa GIZ
ambao walifadhili mafunzo hayo na Jumuia ya Afrika Mashariki.
**********
Na Mtua Salira, EANA
Mshauri
Mtaalamu wa muda mrefu wa Masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) Balozi Jeremy Ndayiziga (54) amefariki dunia baada ya
kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa kisukari mjini Bujumbura,Burundi.
Balozi
huyo raia wa Burundi kwa mujibu wa marafiki wa karibu na ndugu zake
alifariki Jumatano wiki iliyopita na anatarajiwa kuzikwa nchini Burundi
Jumanne ijayo, Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA)
limeripoti.
Kutokana
na hali yake ya afya kuendelea kudorora, Balozi Ndayiziga alilazimika
kukatwa mguu wake wa kulia katika Hopsitali ya Nairobi kutokana
kuzidiwa na ugonjwa wa kisukari na hivyo kubaki hospitalini kwa miezi
ipatayo minne. Afya yake ilionekana kuimarika kidogo na alikuwa
anakaribia kupona.
Mara
ya mwisho alionekana makao makuu ya EAC mjini Arusha, Tanzania katikati
ya Novemba mwaka huu katika mkutano wa Maofisa Mawasiliano wa EAC.
Jina
la Balozi Ndayiziga ni maarufu kwa watendaji wa EAC kutokana na umahiri
wake wa uchapaji kazi,uongozi wa busara na kuwa muumini wa itikadi ya
Shirikisho la EAC. Ndiye aliyeiongoza nchi yake katika harakati za
kujiunga na EAC 2007.
‘’Marehemu
Balozi Ndayiziga alikuwa mtu maarufu, mchapakazi mwenzangu na kwa
kweli, zaidi ya yote alikuwa rafiki yangu wa karibu sana,’’ alisema Jean
Rigi,Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki nchini Burundi na
kuongeza kuwa wengi watamkosa na ni pigo kubwa kwa wote wanaopigania
kujenga Afrika Mashariki na raia wake.
Mkongwe
wa masuala ya habari nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu kufuatia
taarifa ya kifo hicho alisema: ‘’Nimepata mshtuko mkubwa! Nilijua kwamba
alikuwa anaugua lakini nilifikiri kwamba ni jambo la kawaida tu
linaloweza kudhibitiwa.
Nimesikitishwa
sana kwa sababu alikuwa ni mtu makini na mwalimu mwenye uelewa wa hali
ya juu na alikuwa mwakilishi mzuri wa masuala ya mtangamano wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki.Nilifanya naye kazi kwa karibu sana kwa kipindi cha
zaidi ya miaka mitano.’’
Naye
mmoja kati wafanyakazi aliokuwa anafanya nao kazi kwa karibu ni
Sukhdev Chhatbar, Mtaalamu wa Masuala ya Habari, ambaye alielezea
kusitishwa na kifo Balozi Ndayiziga.‘
’Tulikuwa
tunawasiliana vyema katika uekelezaji wa miradi mbalimbali.Alikuwa mtu
maarufu, mwenye msimamo thabiti,mwenye busara na alikuwa tayari kufanya
lolote kuimarisha mchakato wa mtangamano wa kikanda,’’ alisema Chhatbar,
mwandishi wa habari maarufu aliyekuwa anasafiri na kusimamia miradi ya
pamoja ya EAC na marehemu Balozi huyo katika nchi wananchama wa jumuiya.
Marehemu ameacha mjane na watoto wanne.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia