SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIKA SIKU YA KWANZA
Posted by
woinde
on
Friday, December 26, 2014
in
MATUKIO
MATUKIO UTALII
|
|
Desemba 16 mwaka huu Waziri wa Mambo ya nje
ya Nchi ,Mh Benard Membe alikabidhi bendera kwa Balozi Adadi Rajabu
kwa niaba ya Mabalozi ,ikiwa ni ishara ya kuanzisha safari ya kupanda
Mlima Kilimanjaro na safari hiyo ilianza kwa muda wa siku
sita. |
|
Safari ilianza kwa taratibu huku Mabalozi
wakitizama mandhari tofauti ya uoto wa asili katika Mlima
Kilimanjaro. |
|
Safari ya kuelekea Kileleni hivi ndivyo
ilivyoendelea kuchukua kasi kwa Mabalozi . |
|
Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard
Membe akioneshwa moja ya kibao kilichokuwa kikielekeza muelekeo wakati
wa kupanda Mlima Kilimanjaro. |
|
Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard
Membe akipita katika moja ya daraja kuelekea eneo la Nusu
njia. |
|
Baada ya kuongoza msafara wa Mabalozi kama
ishara ya kuanzisha upandaji wa mlima Kilimanjaro kwa
Mabalozi,hatimaye Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard Membe
alifika eneo la Nusu njia. |
|
Waziri wa mambo ya nje ya nchi,Mh Benard
Membe akipata chakula na mkuu wa wilaya ya Rombo ,Elenas Parangyo mara
baada ya kufika katika eneo la Nusu Njia(Kisambioni) |
|
Wageni waliokuwa wakipanda Mlima Kilimanjaro
walipata nafasi ya kupiga picha na Waziri wa mambo ya nje ya
Nchi,Benard Membe. |
|
Mabalozi wakiwa na Waziri wa mambo ya nje ya
nchi,Benard Membe wakipata chakula katika eneo la Nusu
Njia. |
|
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja eneo
la Kisambioni. |
|
Mabalozi wakiwa katia picha ya pamoja na
Waziri wa Mambo ya nje ya nchi ,Benard Membe katika eneo la Kisambioni
,eneo ambalo mh Membe aliwaaga Mabalozi katika safari yao ya kupanda
Mlima Kilimanjaro. |
|
Baada ya kupumzika katika eneo la Kisambioni
na kupata chakula ,safari iliendelea ya kwenda kituo cha
Mandara. |
|
Kila mmoja alikuwa na Morali ya juu wakati
wote wa kupanda Mlima Kilimanjaro. |
|
Wakati mwingine Mabalozi walilazimika
kupumzika na kupoza koo kabla ya kuendelea na safari
. |
|
Baada ya mapumziko safari ya kupanda Mlima
iliiendelea . |
|
Wasaidizi katika kupanda Mlima Kilimanjaro
kutokana na uzoefu walionao ,wao walifika mapema katika kituo cha
Mandara kwa ajili ya Maandalizi . |
|
Baada ya safari ya takribani saa tano
hatimaye ujumbe wa Mabalozi uliwasili kituo cha kwanza cha
Mandara. |
|
Mabalozi baada ya kufika katika kituo cha
kwanza cha Mandara walipata fursa ya kuchukua taswira mbalimbali kwa
ajili ya kumbukumbu. |
|
Baada ya safari ndefu ya kutoka Lango la
Marangu ambako ni mwanzo wa safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro
,Mabalozi walipata chakula cha usiku na kisha kupumzika kwa ajili ya
maandalizi ya siku inayofuata ya kuelekea kituo cha
Horombo. |
|
Globu ya Jamii ikiwakilishwa na mwakilishi
wake kanda ya kaskazini Dixon Busagaga ilishiriki katika safari hiyo
ya Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro ,Tegemea kupata taarifa za
matukio yote tangu kuanza kwa safari hiyo hadi kilele cha Mlima
Kilimanjaro kupitia hapa hapa Globu ya jamii. |
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia