Waziri wa Nishati na Madini akiulizia utekelezaji wa umeme katika
kijiji cha Kamgendi katika siku yake ya kwanza ya siku 6 za ziara katika
Wilaya zote za Mkoa wa Mara
Licha ya watu mbalimbali kutaka Rais Jakaya Kikwete kumwajibisha
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhusiana na
sakata la fedha za escrow, Ikulu imesema suala hilo litatolewa uamuzi
wakati wowote baada ya mapumziko ya sikukuu.
Hivi sasa Rais yupo katika mapumziko ya Sikukuu za
Krismasi inayosherehekewa Desemba 25 kila mwaka na Mwaka Mpya
itakayofanyika Januari Mosi.
Akizungumza na wazee wa Dar es Salaam Desemba 22
mwaka huu, Rais Kikwete alisema amemweka kiporo waziri huyo hadi
atakapopata ufafanuzi wa mambo kadhaa na kwamba atakapojilidhisha
ataujulisha umma.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
aliliambia gazeti hili jana kuwa Rais Kikwete bado hajakamilisha
kulishughulikia suala hilo na kwamba litakapokuwa tayari wananchi
watajulishwa hatua alizozichukua.
“Unakumbuka Rais alichosema? Bado analifanyia
kazi, atakapomaliza tu mtajulishwa, sasa hivi ni kipindi cha sikukuu,”
alisema Sefue.
Profesa Muhongo
Hata hivyo, Profesa Muhongo alipotakiwa
kuzungumzia shinikizo linalotolewa la kutaka ajiuzulu kabla ya Rais
Kikwete kutoa uamuzi wake, aliliambia gazeti hili jana kwa simu kuwa;
“Mimi sasa sitaki kuzungumza na waandishi, mambo yangu yote wapo watu
ambao wanaweza kuyazungumzia.”
Hata hivyo, katika hotuba yake, Rais Kikwete
aliagiza kuchukuliwa hatua kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Eliakimu Maswi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma kuhusu
ushiriki wake kwenye kashfa hiyo.
Siku iliyofuata, Sefue alimweka ‘kando’ Maswi na
kumteua Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava
kukaimu nafasi hiyo hadi uchunguzi utakapokamilika.
Kutokana na kuchelewa kutekelezwa kwa maazimio ya
Bunge yaliyotaka viongozi hao kuwajibishwa, Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) umeahidi kuwasilisha hoja bungeni ya kupiga kura ya kutokuwa na
imani na waziri mkuu na kufanya maandamano nchi nzima.
Mpaka sasa viongozi watatu wameshakumbwa na
dhoruba inayotokana na sakata la escrow baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa
Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema, kung’olewa kwa Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na kuwekwa
kando kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Maswi.
Wapinzani Zanzibar wakoleza moto
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia