Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es
Salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Kushoto
ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik na kulia ni katibu wa
Baraza la wazee wa Dar es Salaam Mzee Mtulia.
Rais Jakaya Kiwete akihutubia taifa hii leo katika ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam kupitia wazee wa jiji hilo.
Rais Jakaya Kiwete akihutubia taifa hii leo katika ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam kupitia wazee wa jiji hilo.
Pampoja
na mambo mbalimbali Rais Kikwete amezungumzia Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa uliofanyika nchini kote na kuunga mkono maamuzi ya Waziri
TAMISEMI, Hawa Ghasia juu ya maamuzi ya kuwatimua kazi, kusimamisha,
kuwashusha vyema na kuwapa maonyo ya madaraja mbalimbali watendaji wote
waliohusika na kuharibika kwa uchaguzi huo katika maeneo yao.
Rais Kikwete hivi sasa anazungumzia sakata la ESCROW ambapo kwa mambo kadhaa ambayo yalikuwa yakisubiri uamuzi wake ikiwa ni pamoja na kuwaondoa mawaziri tajwa.
Rais
Kikwete amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali tayari amejiuzulu, Bodi
ya Tanesco imeshamaliza muda wake na tayari amesha teua Mwenyekiti Mpya
wa Bodi huku Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna
Tibaijuka akisema amesha zungumza nae na amemuomba apishe nafasi yake
ateuliwe mtu mwingine.
Upande
wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameomba amuweke
kiporo yeye na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi kupisha uchunguzi dhidi
yao.
Baadhi
ya wazee na wananchi wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete wakati alipokuwa akilihutubia taifa kupitia wazee wa Dar es
Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.
Wanahabari wakichukua kumbukumbu kwenye mkutano huo wa
Mh.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa
Dar es Salaam leo Desemba 22, 2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es Salaam.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia